LIVE STREAM ADS

Header Ads

NACOPHA yatoa mafunzo kwa watu wanaoishi na VVU

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Kanda ya Mwanza kupitia Mradi wa HEBU TUYAJENGE unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo kutoka kwa Watu wa Marekani (USAID) limetoa mafunzo ya Sheria na Masuala ya Haki Za Binadamu kwa viongozi wa vikundi vya watu watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na WAVIU kutoka Halmashauri 12 za Nyamagana, Musoma, Bukoba, Tabora, Nzega Mji, Nzega wilaya, Igunga, Uyui, Urambo, Sikonge, Kigoma Ujiji na Shinyanga ambapo kati yao waluiohudhuria ni watekelezaji wa mradi ngazi ya jamii, viongozi wa mabaraza ya WAVIU Halmashauri (KONGA) na Waratibu wa UKIMWI wa Halmashauri.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Dkt Leornard Maboko amewapongeza USAID kwa kuiwezesha NACOPHA kuandaa mafunzo hayo ambayo ni muhimu kwa WAVIU na kuwataka washiriki kusambaza maarifa ya haki za binadamu na sheria watakayoyapata kwa jamii ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyapaa.

Kwa upande wao Mwenyekiti wa Baraza, Leticia Mourice na Afisa Mtendaji Mkuu, Deogratius Rutatwa wamesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watu wanaoishi na VVU NA wale wasio na VVU ili wote kwa pamoja watambue haki na wajibu wao.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wamelipongeza shirika la NACOPHA kwa kuandaaa mafunzo hayo ya sheria na masuala ya haki za binadamu na kuomba elimu iendelee kutolewa ili kutokomeza kabisa suala la unyanyapaa ambalo wakati mwingine linasababishwa na WAVIU wenyewe kujinyanyapaa.

Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU kupitia ufadhili wa USAID limendelea kuwajengea uwezo watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ili kuboresha maisha na upatikanaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika jamii.
Na Tonny Alphonce, Shinyanga
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Dkt Leornard Maboko akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi Mkuu NACOPHA akizungumzia mafunzo hayo.

No comments:

Powered by Blogger.