LIVE STREAM ADS

Header Ads

UWT Mwanza: Rais Samia Mitano Tena 2025

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa Mwanza Jumapili Agosti 15, 2021 umefanya maombi maalumu ya kumuombea afya njema na kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha siku 150 za uongozi wake ikiwemo kuendeleza kwa kasi miradi ya kimkakati iliyoasisiwa na mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwa mantiki hiyo, umoja huo kupitia kwa Mwenyekiti wake Hellen Bogohe umesema kuwa zawadi pekee anayostahili Mhe. Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kumuongezea miaka mitano tena kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 ili aendelee kulitumikia Taifa na kuwaletea maendeleo watanzania.

Bogohe amesema kuwa katika Maadhimisho ya Mei Mosi 2021 yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa mgeni rasmi aliahid kupandisha madaraja ya watumishi jambo ambalo ameanza kulitekeleza na watumishi hususani waalimu wamepandishwa madaraja.
Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Mwanza, Mary Mhoha ameelezea ziara ya Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Mwanza ambayo katika hotuba zake ahadi nyingi alizozitoa amezitekeleza ikiwemo kuwateua vijana na wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa inayoendelea mkoani Mwanza.

Mhoha ameongeza kuwa wanawake wa Mkoa wa Mwanza wako bega kwa bega na Mhe. Samiah Suluhu Hassan na wanampongeza kwa kasi kubwa aliyoanza nayo ambapo wanamuombea maisha marefu na afya njema ili aendelee kuleta maendeleo zaidi na kwamba ifikapo 2025 zawadi yao ni kumuongezea miaka mitano tena.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.