LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Bashungwa awasilisha salamu za Rais Samia kwa RAS Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa (juu) amewasilisha salamu za pole za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ndugu Ngusa Samike kufuatia kifo cha Baba yake mzazi Mzee Fredrick Shija Samike.

Waziri Bashungwa amewasilisha salamu hizo katika ibada ya maziko iliyofanyika Januari 25, 2022 katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

"Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amenituma kwa niaba yake na Serikali kutoa salamu za pole kwa familia na ninatoa pole kwa kaka yangu Ngusa kwa pengo kubwa la mzee wetu tulilolipata" amesema Bashungwa.

Waziri Bashungwa ametoa wito kwa ndugu jamaa na marafiki kuendelea kumuombea Mzee Samike huku akisisitiza umuhimu wa wananchi Mjini Kahama na kwingineko kujifunza na kuyaenzi maisha ya mzee Samike.

Aidha, Waziri Bashungwa amepata nafasi ya kutoa mkono wa pole kwa niaba ya Serikali vilevile Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa familia.

Katika msiba huo Waziri Bashungwa ameambatana na Waziri wa Madini Mhe Dkt. Doto Biteko, Naibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis H. Khamis na Wakuu wa Mikoa ya Shinyanga na Mwanza.

Mzee Fredrick Shija Samike alifariki tarehe 20 Januari 2022 katika hospitali ya Bugando iliyopo Jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu na mwili wake umepumzishwa nyumbani kwake Kahama.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akitoa salamu za pole kwa familia Katibu Tawala Mkoa Mwaza, Ngusa Samike baada ya kufiwa na mzee wao, Fredirick Samike.
Mwakilishi wa familia akisoma wasifu wa marehemu Mzee Fredrick Samike aliyezaliwa mwaka 1944 na kufariki mwaka 2022 akiwa na miaka 78 katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza wakati akipatiwa matibabu.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Ngusa Samike (katikati) akiwa na wanafamilia wakati wa ibada ya mazishi ya mzee wao Fredrick Samike aliyefariki duniani Janiuari 20, 2022.
Wanafamilia wakiwa kwenye ibada ya mazishi ya marehemu mzee Fredrick Samike.
Viongozi wa Serikali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Ibada ya mazishi ya marehemu mzee Fredrick Samike imefanyika nyumbani kwake Kahama mkoani Shinyanga.
Waombolezaji mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Waombolezaji.
Waombolezaji.
Viongozi wa Serikali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko (kulia) akimpa pole Katibu Tawala Mkoa Mwanza Ngusa Samike (kushoto) baada ya kufiwa na baba mzazi.
Viongozi mbalimbali wakitoa pole kwa Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Ngusa Samike baada ya kufiwa na baba.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.