LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ilemela waja na mkakati wa kupambana na mimba kwa wanafunzi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Emmanuel Malima,amezinduaujenzi wa bweni la hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari Kilimani,ukiwamkakati wa kukabiliana na mimba za utotoni,utoro kwa wanafunzi wa kike na kuongezaufaulu wao.

Akizindua ujenzi wa msingi wa bweni hilo kisha kuendesha harambee ya ujenzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala, Malima, alisema mradi huo umebuniwana wananchi wenyewe kutokana na mahitaji ya watoto kupata muda wa kujifunza nakujisomea.

Alisemawananchi na jamii wamejitolea nguvu zao, mkuu wa wilaya na mkurugenzi wahalmashauri pia wamejitoa kuhakikisha watoto wa kike wanapata muda wa kujifunzana kujisomea kwenye mazingira mazuri yenye utulivu yatakayosaidia walimu kukuzataaluma na kuongeza ufaulu wa watoto.

Malimaalieleza mahitaji ya mabweni kwenye shule za sekondari ni makubwa na mkakati waidara ya elimu na halmashauri ni kuhamasisha jamii na wananchi kuchangiamiundombinu hiyo ili kupata matokeo chanya kwenye shule za Halmashauri yaIlemela.

Alisema bwenihilo likikamilika watoto watasoma vizuri zaidi tofauti wakitokea nyumbani ambapoaliendesha harambee ya ujenzi wa msingi wa bweni hilo na kuchangia sh. milioni moja kwa niaba ya idara ya elimu Manispaa ya Ilemela.

Mmoja wawadau wa shule hiyo Mhandisi Mnandi Mnandi, alisema kauli mbiu ya Kilimani nikutokomeza sifuri na daraja la nne, hivyo alichangia sh. 350,000 na kuahidikununua viti vya walimu na akawataka wazazi kujitathmini na kuchangia elimu yawatoto wao.
Mwenyekiti waChama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilemela,Nelson Mesha alisema ndicho chenyeilani inayotekelezwa,lazima kione mafanikio kwenye ujenzi wa miundombinu yaelimu na taaluma, lengo sekta ya elimu ipige hatua kubwa.

“Suala la elimu Ilemela imebadilika, Rais Samia Suluhu Hassan ametupunguzia mzigo mkubwana shule hizi ni zetu kwa faida ya watoto wetu na vizazi vyetu,wananchitunaposhirikishwa kwenye miradi hii tuhamasike,hakuna mjomba kutujengea mabwenina madarasa” alisema Mesha.

Alichangiamifuko 10 ya saruji na kuwapongeza walimu,ofisa elimu na halmashauri kwakusimamia elimu kwa weledi hali inayowawezesha walimu kuwaandaa watoto kuwawatalaamu wa baadaye.

Awali Mkuu waShule ya Kilimani,Gerana Majaliwa,alisema mpango wa hosteli ya watoto wa kikeuliridhiwa na wazazi, hivyo ujenzi wa msingi wa bweni hilo litakalokuwa navyumba 20,matundu sita ya vyoo yakiwemo mawili ya wenye mahitaji maalumu na sehemuya kufungulia nguo utagharimu sh. milioni 31.6.

Alisema bweni hilo litachukua wanafunzi zaidi ya 150 na kutokana na mafanikio ya kitaaluma kwa wasichana wanaokaa shuleni ambapo ufaulu wao umeongezeka,nidhamu imeimarika, kupungua kwa idadi ya wanaopata ujauzito, changamoto ya utoro, kuchelewa shuleni sababu ya umbali na usafiri imepungua.

“Mradi wa hosteli ulianza mwaka 2020 ukilenga kupunguza utoro na mimba kwa watoto wa kike ili kuwapa fursa ya kutimiza ndoto zao, kwenye harambee sh.milioni 1.069 taslimu zilikusanywa,ahadi ya fedha sh.milioni 1.6 na mifuko 70 ya saruji” alisema Majaliwa.


Aidha shule ina changamoto ya ukosefu wa bwalo la chakula na jiko, uzio, matundu ya vyoo naviti vya walimu ambapo mfadhili The Desk & Chair Foundation amejitolea kujenga matundu 20 na uongozi unasubiri kusaini mkataba mradi huo uanze.


Alieleza kuwauongozi wa Kilimani Sekondari unampongeza Rais Samia kwa kuthamini elimu nakuipatia Sh. Milioni 40 za vya vyumba viwili vya madarasa na samani (viti nameza) pia Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala kwa kuridhia kuzindua ujenziwa msingi wa hosteli ya wasichana.


“Kipekee tunawashukurumkuu wa wilaya kwa kupambana na kusaidia kutatua changamoto ya majishuleni,Mbunge wa Ilemela, Dkt. Angeline Mabula na Mkurugenzi wa Manispaa,MhandisiModest Apolinary,Chama Cha Mapinduzi kwa michango na maelekeo mazuri,wajumbe wabodi, walimu, wazazi na wanafunzi” alisema Majaliwa.


Baadhi yawanafunzi wa hosteli, Getruderose Joseph wa kidato cha nne na Nuryat Mohamed wakidato cha kwanza, walisema kuishi hosteli ni tofauti na nyumbani, kumewaongezea ari ya kujifunza zaidi sababu ya madhari na mazingira tulivu ya kujifunzia.

No comments:

Powered by Blogger.