LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uchunguzi wabaini chanzo cha vifo vya samaki Mto Mara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Utafiti wa awali uliofanywa na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB) umebaini kuwa kuwepo kwa kiwango cha mafuta aina ya 'oili na grisi' umeathiri uhai wa viumbe hai ikiwemo vifo vy samaki katika Mto Mto unaomwaga maji yake Ziwa Victoria.

Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Renatus Shinhu ameyasem hayo Machi 12, 2022 wakati akizungumza na wanahabari kufuatia tukio la vifo vya samaki katika Mto Mara lililoripotiwa Machi 08, 2022 ambapo ameongeza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini chanzo cha uwepo wa mafuta katika Mto huo.
Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Renatus Shinhu ametoa rai kwa wananchi kutunza vyanzo vya maji katika Bonde la Ziwa Victoria ikiwemo Mto Mara na kujiepusha na shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo zinazochafua mto huo.
Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Renatus Shinhu akizungumza na wanahabari jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini 

No comments:

Powered by Blogger.