LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shughuli za kilimo zahatarisha mradi wa maji Kigongo, Misungwi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wananchi katika Kijiji cha Bukumbi Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wametakiwa kusitisha shughuli za kilimo katika eneo linalozunguka chanzo cha mradi wa maji Kigongo unaotarajiwa kluanza utekelezaji wake mwezi Machi mwaka huu kwa gharama ya shilingi Bilioni 5.2.

Meneja wa Wakala Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Misungwi, Eng. Marwa Kisibo ametoa agizo hilo wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo hilo ili kutunza mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo huadhimishwa Machi 16-22 kila mwaka.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.