LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkandarasi akabidhi Stendi ya Nyamhongolo. RC apigwa butwaa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkandarasi kampuni ya STECOL Corparation ya nchini China amekabidhi kwa Serikali mkoani Mwanza mradi wa Kituo cha Mabasi na Maegesho ya Malori Nyamhongolo ulichopo Manispaa ya Ilemela.

Zoezi la kukabidhi mradi huo uliogharimu shilingi bilioni 26.6 hadi kukamilika limefanyika Machi 09, 2022 ambapo hatua inayofuata ni hafla ya uzinduzi rasmi inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni huku wananchi na wafanyabiashara wakitakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika mradi huo.

Akipokea mradi huo, Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo stendi ya Nyamhongolo ambayo iliasisiwa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa kampuni ya STECOL iliyojenga stendi ya Nyamhongolo wakati wa zoezi la kupokea mradi huo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya Ilemela Hassan Masala (kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali wakikagua stendi ya Nyamhongo.
Jengo la Hostel katika stendi ya Nyamhongolo mahususi kwa ajili ya abiria kulala.
Eneo la Hosteli pamoja na maegesho ya Malori katika Stendi ya Nyamhongolo.
Mwonekano wa jengo la mbele (Bus Terminal) katika Stendi ya Nyamhongolo.
Mwonekano wa jengo la kibiashara (Business Terminal) katika Stendi ya Nyamhongolo.
Mwonekano wa maegesho ya magari madogo chini ya jengo la kibiashara katika stendi ya Nyamhongolo (Underground Parking)
Viongozi na Watendaji mbalimbali wilayani Ilemela wakiwa kwenye hafla fupi ya Mkandarasi kukabidhi Stendi ya Nyamhongolo kwa Serikali mkoani Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.