LIVE STREAM ADS

Header Ads

TCRA kutoa Bure Masafa na Namba Maalum kwa Watafiti

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Afisa Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Aika Benson akimpa maelezo ya shughuli za mamlaka kwa mteja aliyetembelea maonesho ya Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma.
***

Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeanza kutoa masafa pamoja namba maalum za kutoa huduma bure kwa watafiti wote watanzania wanaofanya tafiti zinazolenga katika kutumia Teknolojia ya Mawasiliano kuongeza tija katika shughuli mbalimbali nchini.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu nchini yaliyofanyika jijini Dodoma, Afisa Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano wa TCRA, Mabel Masasi alisema utaratibu huo unalenga katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha ufanyaji wa tafiti ambazo zinalenga katika kuleta maendeleo nchini.

Akizungmzia jinsi ya kupata masafa na namba kwa ajili ya utafiti, Mabel alisema iwapo watafiti wanafanya utafiti kupitia vyuo basi vyuo vyao vinatakiwa kuwasiliana na Mamlaka hiyo ili kuweza kukamilisha taratibu za kupata masafa au namba ya kufanyia utafiti bila kulipia.

Kuhusu watafiti binafsi wanaotaka kufanya utafiti kwa kutumia rasilimali hiz,o Mabel alisema watafiti binafsi watatakiwa kwenda kujisajili Costech ambapo kupitia wao wataweza kuombewa rasilimali hizo kwa ajili ya utafiti bila kulipia.

Madhimisho ya Wiki ya Ubunifu kitaifa yalianza jijini Dodoma kuanzia Mei 15-20, 2022 yakiwa na kaulimbiu isemayo "Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu".
Afisa Mkuu Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi akimpa maelezo ya shughuli za mamlaka kwa mteja aliyetembelea Maonesho ya Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma.
Wanafunzi wakiwa katika banda la TCRA katika Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yaliyofanyika jijini Dodoma.

No comments:

Powered by Blogger.