LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau, jamii waadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Tanzania imeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, Juni 05, 2022 ambapo shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo kufanya usafi pamoja na kupanda miti ili kuendelea kuimarisha uoto wa asili.

Kitaifa maadhimisho hayo yalifanyika jijini Dodoma ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi na alitumia fursa hiyo kuzindua Mpango Kabambe wa Uhifadhi wa Mazingira huku akizitaka mamlaka nchini kusimamia utunzaji wa mazingira ikiwemo utupaji ovyo taka za plastiki ambazo zimekuwa na athari kubwa hususani kwa viumbe hai majini.
Jijini Mwanza, Shirika la usimamizi wa mazingira na utunzaji rasilimali za uvuvi (EMEDO) liliwakutanisha wananchi, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT pamoja na viongozi mbalimbali ngazi za Mtaa kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi katika mitaa na fukwe za Ziwa Victoria Mtaa wa Sweya pamoja na kushiriki mdahalo uliofanyika katika ofisi za shirika hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa EMEDO, Editrudith Lukanga alisema jitihada za shirika hilo kuelimisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira pamoja na kuwezesha vikundi mbalimbali kukusanya takaghafi kama chupa za plastiki zimesaidia kuweka hali ya mazingira katika hali ya usafi.

Nao washiriki wa mdahalo huo waliojengewa uwezo na shirika la EMEDO walisema awali wakati wanaanza kuelimisha jamii kwa kupita kaya kwa kaya, kulikuwa na changamoto ya utapaji taka ovyo zikiwemo taulo za kike zilizotumika (pedi) madaso ya watoto pamoja na chupa za plastiki lakini hali hiyo imepungua baada ya elimu kutolewa.
Wadau wakiongozwa na Shirika la EMEDO wakifanya usafi jijini Mwanza.
Usafi ukendelea katika Mtaa wa Sweya jijini Mwanza
Dunia ni Moja, Tanzania ni Moja, Tunza Mazingira.
#BMGHabari

No comments:

Powered by Blogger.