LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maafisa wa TANESCO wakitoa elimu kwa umma kupitia Jembe FM Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuadhimisha Wiku ya Wateja Duniani kuanzia Oktoba 03-7, 2022, timu ya wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa Mwanza, imepanga kuwafikia wateja wake na kuwaelimisha kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari.

Njia nyingine itakayotumika kuwafikia wateja na kuwahudumia ni kwenye maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza kutembelea maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu ikiwemo masoko na stendi za magari.

Akizungumza jumatatu Oktoba 03, 2022 katika kipindi cha Sega la Leo ndani ya redio Jembe FM, Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga amesema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha wateja wanafurahia huduma bora.

"Tukiwa tunafurahia Wiki ya Wateja Duniani, TANESCO tunakuja kitofauti na mfumo mpya wa kidijitali wa Ni-Konekt ambapo wataweza kufanya maombi ya kuunganishiwa umeme kupitia simu ya mkononi" amesema Kayaga.

Naye Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Joyce Makori amesema shirika hilo limekuja na mfumo wa pamoja uitwao CRM (Custumer Relationship Managment) utakaowezesha wateja kutoa taarifa mbalimbali bila usumbufu kama ilivyokuwa hapo awali ambapo njia iliyokuwa ikitumika ilikuwa ikilalamikiwa kuelemewa (busy) na haikuwa ikitunza kumbukumbu namna mteja amehudumiwa.

Ili kupata huduma ya Ni-Konekt mteja anapaswa kuwa na namba ya kitambulisho cha NIDA ambapo anaweza kuingia kwenye tovuti ya TANESCO (www.tanesco.co.tz), kupakua App ya Nikonect kwa watumiaji wa simu janja ama kupiga *152*00# kwa watumiaji wa simu za viswaswadu na watakaohitaji msaada zaidi watawasiliana na TANESCO kupitia simu nambari 0748 55 00 00.

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, timu ya TANESCO Mkoa Mwanza kuanzia jumatatu Oktoba 03 hadi Ijumaa Oktoba 07, 2022 itakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo kuwatembelea wateja, kutoa elimu na kutatua changamoto zao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Afisa Masoko Mwandamizi TANESCO Mkoa Mwanza, Flaviana Moshi (kushoto) akiwa na Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayagi (kulia) katika kipindi cha redio Jembe FM kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2022.
Maafisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Johari Mrisho (kushoto) na Joyce Makori (kulia) wakiwa redio Jembe FM kuelimisha umma kuhusiana na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.
Watangazaji wa Jembe FM wakifanya mazungumzo na maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.