LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wateja wa TANESCO wahimizwa kutumia Ni-Konekt kupata huduma kwa haraka

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamehimizwa kutumia huduma mpya ya kidijitali iitwayo Ni-Konekt ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo kutoa taarifa za dharura pamoja na maombi mapya ya kuunganishiwa umeme kwa haraka bila usumbufu.

Afisa Masoko Mwandamizi TANESCO Mkoa Mwanza, Flaviana Moshi ametoa rai hiyo Jumatatu Oktoba 03, 2022 wakati akizungumza katika kipindi cha Asubuhi Njema cha Radio Iqra FM ya jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.

Moshi amesema huduma hiyo pia inaondoa urasimu na mianya ya vishoka na kuongeza ufanishi wa upatikanaji wa huduma ya umeme huku ikiokoa muda wa mteja kufuatilia maombi yake.

Ili kupata huduma ya Ni-Konekt mteja anapaswa kuwa na namba ya kitambulisho cha NIDA ambapo anaweza kuingia kwenye tovuti ya TANESCO (www.tanesco.co.tz), kupakua App ya Nikonect kwa watumiaji wa simu janja ama kupiga *152*00# kwa watumiaji wa simu za viswaswadu.

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, timu ya TANESCO Mkoa Mwanza kuanzia jumatatu Oktoba 03 hadi Ijumaa Oktoba 07, 2022 itakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo kuwatembelea wateja, kutoa elimu na kutatua changamoto zao.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga akieleza manufaa ya mfumo wa Ni-Konekt akishiriki kipindi cha asubuhi njema redio Iqra FM
Timu ya TANESCO Mkoa Mwanza ikiwa redio Iqra FM Mwanza kutoa elimu kwa umma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2022.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Joyce Makori akihimiza matumizi ya nambari 0748 55 00 00 kwa ajili ya wateja kutoa taarifa mbalimbali.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Joyce Makori (kulia) akiwa redio Iqra FM.
Aisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Johari Mrisho akitoa elimu ya usalama wa umeme kwa wateja wa TANESCO hususani kutosogelea nyaya zizilizokatika, matawi ya miti yaliyousana na nyaya za umeme na kutofanya shughuli za kibinadamu katika maeneo yenye miundombinu ya umeme.

No comments:

Powered by Blogger.