LIVE STREAM ADS

Header Ads

PICHA: Matembezi ya miaka 40 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi (CDTTI)

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (CDTTI) wameshiriki matembezi ya miaka 40 tangu kuanzisha Chuo hicho mwaka 1982.

Matembezi hayo yamefanyika Disemba 06, 2022 majira ya asubuhi yakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Charles Achuodho na kupokelewa na Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi, Petro Sabatto kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy.

Shughuli mbalimbali pia ambazo zitafanywa na Chuo hicho katika kuadhimisha miaka 40 ni pamoja na kupanda miti chuoni, kushirikiana na jamii kuzibua barabara ya Mbela, maonesho ya wajasiriamali, mdahalo (Disemba 07, 2022) pamoja na mahafali yatakayofanyika Disemba 08, 2022.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama picha zaidi kuhusiana na matembezi hayo yaliyoambatana na Baraka ya mvua.
Katibu Tawala Wilaya Misungwi, Petro Sabatto (kushoto) akipokea matembezi hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy.
Katibu Tawala Wilaya Misungwi, Petro Sabatto (wa tatu) akiongoza matembezi kuelekea barabara ya Mbela kushiriki ujenzi wa barabara hiyo ambao umeasisiwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (CDTTI) kama sehemu ya mchango wake katika jamii katika kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa.
Katibu Tawala Wilaya Misungwi, Petro Sabatto (kulia), Mkuu wa Chuo cha CDTI, Charles Achuodho (wa pili kulia) na wanafunzi wa Chuo hicho wakishiriki ujenzi wa barabara ya Mbela wilayani Misungwi.
Endelea kukaa karibu na BMG BLOG kujionea matukio zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.