LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya TOMA yakaribisha wanachama wapya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com 
Taasisi ya waandishi wa habari za mtandaoni (Tanzania Online Media Alliance- TOMA) imewahimiza imefungua milango kwa wanachama wapya kujiunga na taasisi hiyo ili kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo yatakayowawezesha kutimiza majukumu yao kwa weledi zaidi.

Mratibu wa taasisi hiyo, Seif Mangwangi aliyasema hayo Machi 28, 2023 wakati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari wa mtandaoni jijini Mwanza katika kikao kifupi cha kuitambulisha taasisi hiyo.

Alisema taasisi hiyo imelenga kuhakikisha waandishi wa habari za mtandaoni wanafanya kazi kwa weledi kwa kuwajengea uwezo kupitia mafunzo mbalimbali pamoja na kuhakikisha inatetea maslahi na haki zao inapotokea changamoto mbalimbali.

Mangwangi aliwahimiza waandishi wa habari za mtandaoni kutembelea tovuti ya TOMA ambayo ni www.toma.or.tz kutuma maombi ya kujiunga na taasisi hiyo ambayo ilizinduliwa mwezi Februari 2023 jijini Dodoma.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Alex Gwido ambaye alisema taasisi hiyo imekuja wakati mwafaka na kushauri kuwasaidia waendeshaji wa mitandao ya kijamii ili kunufaika na ujira unaotolewa na makampuni ya mitandao ya kijamii ikiwemo Google kupitia matangazo mbalimbali.
Mratibu wa taasisi ya TOMA, Seif Mangwangi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari za mtandaoni jijini Mwanza.
Wanahabari wa mtandaoni jijini Mwanza wakimsikiliza Mratibu wa taasisi ya TOMA, Seif Mangwangi (kulia).

No comments:

Powered by Blogger.