LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la TAHEA Mwanza lahimiza wadau kushirikiana kuwalinda watoto

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Uchumi wa Nyumbani (Tanzania Home Economics Organization- TAHEA) Mwanza limewahimiza wadau mbalimbali kushirikiana kwa pamoja ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto hatua itakayosaidia kuwanusuru pia na vitendo vya ukatili.

Rai hiyo imetolewa Jumanne Mei 30, 2023 jijini Mwanza kwenye kikao kazi cha ulinzi na usalama wa mtoto kilichoandaliwa na shirikika hilo na kuwashirikisha maafisa wa jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia pamoja na waandishi wa habari.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mratibu wa Miradi ya Watoto kutoka TAHEA Mwanza, Damas Joachim amesema wadau wa masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto wakifanya kazi kwa ushirikiano, watasaidia kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya watoto.

"Maafisa wa polisi kupitia dawati ya jinsia na watoto ndio wanapokea na kuratibu taarifa mbalimbali za awali kuhusiana na matukio ya ukatili dhidi ya watoto hivyo tumeona ni vyema kuwashirikisha katika jitihada za kuwalinda watoto" amesema Joachim.

Joachim amebainisha kuwa katika kuimarisha malezi na makuzi bora ya watoto, shirika la TAHEA limezindua jarida maalum la Mbeleko ambalo linatolewa bure kwa wazazi na walezi ili kuwasaidia kutambua mbinu sahihi za malezi ya watoto.

"Wazazi na wana nafasi kubwa ya malezi na makuzi bora kwa watoto hivyo hawapaswi kukwepa wajibu huo kwa kisingizio cha majukumu. Pia mtoto akikosa malezi bora katika kipindi cha miaka nane ya ukuaji wake inaweza kuathiri maisha yake ya baadae. Pia katika kipindi cha miaka miwili ya awali kwenye ukuaji wake akikosa lishe bora anaweza kudumaa na kushindwa kuleta tija katika maisha yake ya baadae" amebainisha Joachim.

Naye Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mwanza, Faraja Mkinga amesema watoto wamekuwa katika hatari ya kukabiliana na matukio mbalimbali ya ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti kutoka kwa watu wa karibu hivyo ni vyema wazazi na walezi wakaimarisha jitihada za kuwalinda na matukio hayo.

Kwa upande wake Mhariri Mshauri wa jarida la Mbeleko, Abubakar Karsan amesema wadau wa ulinzi na usalama wa mtoto ambao ni pamoja na mashirika ya kijamii kama TAHEA, waandishi wa habari na jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia wakiimarisha ushirikiano watoto watakuwa salama katika jamii.

"Nikiwa nafanya kazi ya uandishi wa habari, nilipata taarifa ya mtoto kuhukumiwa kifungo cha maisha kimakosa, nilishirikiana vyema na vyombo vya ulinzi ikiwemo jeshi la polisi na mahakama na tukafanikiwa kumtoa gerezani na leo hii ni wakili, bila ushirikiano wa pamoja tusingeweza kumsaidia" amesema Karsan akihimiza wadau kushirikiana kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mtoto.

Kwa mujibu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, mwaka 2022 kulikuwa na matukio 12,163 ya ukatili dhidi ya watoto ambapo kati ya hayo, matukio 9,962 walikuwa watoto wa kike na 2,201 walikuwa watoto wa kiume.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mratibu wa Miradi ya Watoto (Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali Watoto) kutoka Shirika la Uchumi wa Nyumbani (Tanzania Home Economics Organization- TAHEA) Mwanza, Damas Joachim akizungumza wakati wa kikao kazi cha ulinzi na usalama wa mtoto kilichofanyika Jumanne Mei 30, 2023 jijini Mwanza.
Mratibu wa Miradi ya Watoto kutoka Shirika la TAHEA Mwanza, Damas Joachim akizungumza kwenye kikao hicho ambacho pia kimelenga kuimarisha mahusiano baina ya TAHEA na maafisa wa jeshi la polisi ili kufanya kazi kwa ukaribu zaidi katika kuwalinda watoto.
Wadau wa malezi malezi na makuzi ya watoto jijini Mwanza wakiwa kwenye kikao kazi cha ulinzi na usalama wa mtoto. Washiriki wamekubaliana kushirikiana pamoja pia katika uandaaji wa taarifa za jarida la Mbeleko linaloelimisha wazazi na walezi kuhusu makuzi na makuzi bora ya watoto.
Mratibu wa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la TAHEA Mwanza, Peter Matyoko akiwasilisha mada kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la TAHEA Mwanza, Peter Matyoko akiwasilisha mada kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mstaafu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan ambaye pia ni Mhariri Mshauri wa jarida la Mbeleko linaloandaliwa na shirika la TAHEA Mwanza kwa ajili ya kutoa mwongozo wa malezi na makuzi ya watoto akizungumza kwenye kikao hicho.
Wadau wakiwa kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mstaafu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan ambaye pia ni Mhariri Mshauri wa jarida la Mbeleko linaloandaliwa na shirika la TAHEA Mwanza kwa ajili ya kutoa mwongozo wa malezi na makuzi ya watoto akizungumza kwenye kikao hicho.
Wadau wakiwa kwenye kikao hicho.
Wadau wakisoma jarida la Mbeleko linaloandaliwa na shirika la TAHEA Mwanza kwa ajili ya kutoa mwongozo wa malezi na makuzi ya watoto.
Wadau wakisoma jarida la Mbeleko linaloandaliwa na shirika la TAHEA Mwanza kwa ajili ya kutoa mwongozo wa malezi na makuzi ya watoto.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho.
Wadau wakisoma jarida la Mbeleko linaloandaliwa na shirika la TAHEA Mwanza kwa ajili ya kutoa mwongozo wa malezi na makuzi ya watoto.
Mratibu Miradi Shirika la TAHEA Mwanza, Julieth Joseph akifuatilia hoja mbalimbali wakati wa kikao hicho.
Afisa Mradi wa Watoto Wetu, Tunu Yetu kutoka Shirika la TAHEA Mwanza, Farida Mzimbiri akifuatilia kikao hicho.
Mratibu wa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la TAHEA Mwanza, Peter Matyoko akifuatilia hoja kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la TAHEA Mwanza, Peter Matyoko akiwasilisha mda kwenye kikao hicho.
Picha ya pamoja.
SOMA PIA>>> Shirika la TAHEA lazindua Jarida la Malezi ya Watoto

No comments:

Powered by Blogger.