LIVE STREAM ADS

Header Ads

MANDONGA ataka kuzichapa na GOLOLA wakipima uzito Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Takribani mabondia 20 wanatarajiwa kupanda ulingoni kwenye pambano la Usiku wa Vitasa Jumamosi Julai 29, 2023 katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza.

Wakipima afya na uzito Julai 28, 2023 katika uwanja wa Furahisha, mabondia hao kila mmoja ametamba kuibuka na ushindi huku tambo zaidi zikiwa ni kati ya Karim Mandonga wa Tanzania na Moses Golola wa Uganda.

Usiku wa Vitasa Mwanza utaongozwa na pambano la kuwania mkanda wa WBF kati ya bondia mtanzania Twaha Kiduku na bondia kutoka Afrika Kusiki, Asemahle Wellem.

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa katika vituo mbalimbali jijini Mwanza pamoja na Malaika Bearch Resort kwa gharama ya shilingi 30,000, shilingi 50,000 na shilingi 100,000. 
Kwa mahitaji ya tiketi piga simu nambari 0767 94 15 97.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.