LIVE STREAM ADS

Header Ads

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara akutana na Mkurugenzi Mkuu WIPO

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah (kushoto) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia kulinda hakimiliki za ubunifu duniani (WIPO), Daren Tang (kulia) makao makuu ya shirika hilo mjini Geneva, Uswisi, tarehe 13 Septemba 2023.

Mazungumzo yao yamelenga kuimarisha ulinzi wa haki miliki za ubunifu na ushirikiano wa kimataifa ambapo Dkt. Abdallah amemshukuru Tang kwa ushirikiano mkubwa ambao WIPO imekuwa ikiutoa, ikiwemo ushauri wa kitaalamu kuhusu uanzishwaji wa Sera ya Taifa ya haki miliki na ubunifu Tanzania bara, kuanzishwa kwa sera ya haki miliki na ubunifu Zanzibar na kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini Tanzania.

Tang ameipongeza Tanzania kwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mradi wa hakimiliki nchini

No comments:

Powered by Blogger.