LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dkt. Biteko atembelea banda la Barrick kwenye mkutano wa uwekezaji katika sekta ya madini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akipata maelezo ya utendaji wa kampuni ya Barrick kutoka kwa Makamu wa Rais wa wa Utafiti wa Madini wa Barrick Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Nathan Komarnisky alipotembelea banda la Barrick kwenye Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa katika Sekta ya Madini jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Makamu wa Rais wa Utafiti wa Madini wa Barrick Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Nathan Komarnisky alipotembelea banda la Barrick kwenye Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa katika Sekta ya Madini. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.
Waziri wa Madini, Antony Mavunde akisalimiana na Makamu wa Rais wa Utafiti wa Madini wa Barrick Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Nathan Komarnisky.
Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido akieleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Twiga katika kukuza uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya wananchi.
Washiriki mbalimbali wakitembelea banda la maonesho la Barrick na Twiga.
Washiriki mbalimbali wakitembelea banda la maonesho la Barrick na Twiga.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick wanaoshiriki katika mkutano huo.
***

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, DkT. Doto Biteko ametembelea banda la maonesho la kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick inayoendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga katika Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa katika Sekta ya Madini jijini Dar es salaam.

Dkt. Biteko amepata maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni kupitia migodi Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi pamoja na mafanikio yaliyopatikana tangu Barrick ianze kuendesha shughuli za migodi nchini.

Dkt. Doto Biteko amekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Meneja Mkuu wa Barrick nchini, Melkiory Ngido ametoa wasilisho katika mkutano huo wa kimataifa na kubainisha mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Twiga nchini katika uchimbaji wa madini ambao umefanikisha kuleta mapinduzi mbalimbali yenye tija.

Mapinduzi hayo ni pamoja na kutoa mchango katika pato la Taifa, kuongeza fursa za ajira kwa watanzania, kutekeleza miradi ya huduma za kijamii kupitia sera ya CSR, kuboresha sekta ya elimu na kuinua maisha ya wazabuni wa kitanzania.

No comments:

Powered by Blogger.