LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mahafali Shule ya Sekondari Ole Njoolay yafanya, Mwenyekiti UVDS awakosha wahitimu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shule ya sekondari ya Ole Njoolay iliyopo Kata ya Isamilo jijini Mwanza imefanya mahafali ya 16 ya kidato cha nne huku mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Makondakta jijini Mwanza (UVDS), Mlimi Juma akitoa ahadi kedekede.

Mahafali hayo yamefanyika Ijumaa Oktoba 27, 2023 katika viunga vya shule hiyo yakipambwa na burudani pamoja na maonesho ya kitaaluma kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajiwa kufanya mitihani yao ya mwisho mwaka huu.

Akizungumza kwenye mahafali hayo, mgeni rasmi ametoa ahadi ya kutatua changamoto ya ukosefu wa mashine ya kutolea nakala (photocopy machine) katika shule hiyo ili kurahisisha shughuli mbambali za ufundishaji.

"Siku ya kukabidhi mashine hiyo, pia nitakabidhi jenzi na mpira kwa ajili ya kuhamasisha michezo hapa shuleni" amesema Mlimi  huku akishangiliwa kwa furaha.

Pia mgeni rasmi amesema ikiwa wanafunzi wa kidato cha nne watafanya vizuri katika mtihani wao wa kitaifa, ataandaa sherehe ya kuwapongeza wakiwa na waalimu wao itakayofanyika nje ya viunga vya shule hiyo ili wafurahie ushindi kwa pamoja.

Katika hatua nyingine amewaasa wazazi kuendelea kuwalea watoto wao katika malezi bora wakati wakisubiri matokeo ya kidato cha nne ili ndoto zao za kupata elimu zisije kuzimwa wakati wakisubiri matokeo.

Mkuu wa shule ya sekondari Ole Njoolay, Mwl. Josephat George amesema jumla ya wanafunzi 137 wanatarajiwa kufanya mtihani wao wa kidato cha nne katika shule hiyo na kwamba wanafunzi wameandaliwa vyema kitaaluma ili kufanya vizuri.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Chama cha Makondakta jijini Mwanza (UVDS), Mlimi Juma akivalishwa skafu baada ya kuwasili katika mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Ole Njoolay jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Makondakta jijini Mwanza (UVDS), Mlimi Juma akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa shule ya sekondari Ole Njoolay, Mwl. Josephat George akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Chama cha Makondakta jijini Mwanza (UVDS), Mlimi Juma akishiriki zoezi la upandaji miti katika shule ya sekondari Ole Njoolay.
Mwenyekiti wa Chama cha Makondakta jijini Mwanza (UVDS), Mlimi Juma akishiriki zoezi la upandaji miti katika shule ya sekondari Ole Njoolay.
ZOezi la upandaji miti likiendelea.
Mwenyekiti wa Chama cha Makondakta jijini Mwanza (UVDS), Mlimi Juma (wa pili kulia) akishiriki zoezi la ukataji keki.
Mwenyekiti wa Chama cha Makondakta jijini Mwanza (UVDS), Mlimi Juma akilishwa keki.
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.