LIVE STREAM ADS

Header Ads

TANESCO watamba mashindano ya Mei Mosi 2024

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeshiriki mashindano ya Mei Mosi 2024 yanayooendelea mkoani Arusha.

Timu za shirika hilo ambazo ni timu ya mpira wa miguu na mpira wa pete zimefanikiwa kufuzu robo fainali huku mpira wa wavu (Me & Ke) na riadha mita 200 imefuzu nusu fainali na kufanikiwa kutinga fainali ya riadha mita 100 huku ikishika nafasi ya nne katika mchezo wa vishale (Darts) na mshindi wa pili katika mchezo wa drafti ambao uliwakilishwa na mchezaji Mussa Khalfan.

Mashindano haya yalizinduliwa rasmi Aprili 20, 2024 na mechi kati ya TANESCO na Ulinzi ambapo timu ya Ulinzi ilishinda bao mbili (2) na timu ya Tanesco kuambulia bao moja (1) katika mchezo wa mpira wa miguu.

Mwenyekiti wa michezo TANESCO, Nsajigwa Samuel amesema "Hali ya wachezaji kambini ni nzuri na salama. Kama timu tuna malengo makubwa ya kutwaa ubingwa wa michezo hii ambayo tumefanikiwa kufuzu hatua mbalimbali kwani sio mara ya kwanza kubeba vikombe, hivyo tunayo nia na tunao uwezo wa kufanikisha malengo yetu".
Nazo timu za taasisi mbali mbali zinaendelea kutunishiana misuli ambapo katika mpira wa miguu TANESCO itachuana na TANROADS, huku mpira wa pete (Netball) TANESCO itakutana na timu ya Ikulu kwenye hatua ya robo fainali na mpira wa wavu (Ke) watachuana na timu ya Uchukuzi katika hatua ya nusu fainali.
Imeandaliwa na Na Prisca Kayaga, Arusha.

No comments:

Powered by Blogger.