Rais Samia mgeni rasmi siku ya kupiga vita dawa za kulevya kitaifa jijini Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda amewahimiza wananchi kujitokeza kwenye maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya yaliyoanza tarehe 28- 30 Juni 2024 katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Mtanda amesema maadhimisho hayo yataambatana na utoaji elimu kuhusu masuala ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya huku Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho hayo, Juni 30, 2024.
Wadau mbalimbali wameungana na mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Tanzania (DCEA) kushiriki maadhimisho hayo ambayo yameambatana na kaulimbiu isemayo “wekeza kwenye kinga na tiba dhidi ya dawa za kulevya”.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA
No comments: