LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Mtwara atembelea visima vya gesi Ntorya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Mtwara, Mwanahamisi Munkunda akiwa katika ziara kisi ma cha Ntorya-2 Kata ya Nanguruwe.
Meneja mradi wa gesi asilia Ntorya, Patrick Kabwe akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,  alipotembelea kisima cha gesi Ntorya 1.
***


Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mwanahamisi Munkunda amefanya ziara ya kutembelea visima vya gesi asilia (Ntorya 1 na Ntorya 2) katika Kata ya Nanguruwe ili kujionea maendeleo ya visima hivyo.

Akizungumza katika ziara hiyo, Munkunda alipongeza uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuwa thabiti kwenye shughuli za utafutaji na uendelezaji wa nishati ya gesi asilia pamoja na kuwa wa mfano kwenye utekelezaji wa miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii ‘CSR’ mkoani Mtwara.

"Nawapongeza TPDC kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya gesi mkoani Mtwara, kwetu sisi ni fursa kwani wananchi wanapata ajira, kuongeza pato la halmashauri kupitia Mrabaha pamoja na uboreshwaji wa huduma za kijamii kupitia CSR mfano mzuri ni ujenzi wa kituo cha Afya cha Msimbati" alisema Munkunda.

Meneja mradi Patrick Kabwe alieleza kuwa licha ya maendeleo ambayo yamefanyika katika visima hivyo viwili, TPDC na kampuni ya ARA wanakusudia kuchimba kisima cha tatu cha Chikumbi-1 ili kuongeza uzalishaji wa gesi asilia.

‘‘Sasa hivi tunakusudia kuanza uzalishaji wa gesi asilia kwa awamu , awamu ya kwanza ya uzalishaji tunategemea kuanza mwezi Aprili, 2025, pamoja na hayo kutakuwa na uchorongaji wa kisima cha Chikumbi-1 katika kijiji cha Namahyakata barabarani ambapo visima vyote vitatu (03) vikiwa kwenye uzalishaji vitazalisha hadi futi za ujazo milioni 60 kwa siku’’ alisema Kabwe.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mwanahamisi Munkunda akizungumza na wananchi 
Wananchi wa Nanguruwe wakifuatilia mkutano huo.

No comments:

Powered by Blogger.