LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mufindi wahimizwa kutumia nishati safi ya kupikia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wakazi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kufanya kweli katika matumizi ya nishati safi ya kupikia na kutobaki nyuma kwa kutumia nishati isiyokuwa safi.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dkt. Linda Salekwa wakati wa mkutano uliofanyika jana katika Kata ya Ifwagi.

Dk Salekwa anasema wakazi wa Mufindi wanatakiwa kuhamia katika nishati safi ya kupikia kwa kununua majiko ya gesi au umeme.

"Kuanzia ngazi ya familia, tusibaki nyuma kabisa katika kutumia nishati safi. Ni wakati wetu huu wa kufanya kweli" amesema.
Katika hatua nyingine, Dkt. Salekwa amewaagiza wababa wa wilayani Mufindi kutenga muda na kuzungumza na mabinti zao masuala ya kuhusu hedhi salama.

"Ni wakati sasa wababa wa wilaya yetu kuweza kuzungumza na binti zao ili kuweza kuvunja ukimya na kuwafundisha kuhusu hedhi salama" amesema.

Naye mkazi wa Kata ya Ifwagi, Faraja Peter ameahidi kuwa ataendelea kuhamasisha wakazi wenzake wa kata ya Ifwagi kuweza kutumia vyoo bora pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Ifwagi, Xavery Fute amesema wao kama Serikali ya Kata watafanya tathimini na kuangalia ni kaya zipi ambazo hazijakamilisha zoezi la ujenzi wa vyoo bora.

No comments:

Powered by Blogger.