APOT yaomba Serikali kusaidia taaluma ya viungo tiba
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais wa Chama cha Wataalamu wa Viungo na Vifaa Tiba Saidizi Tanzania (APOT), Dkt. Exaud Kasegezya ameiomba Serikali kusaidia upatikanaji wa taaluma ya viungo tiba nchini ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa wataalamu hao.
Dkt. Kasegezya alitoa ombi hilo Oktoba 05,2024 jijini Mwanza kwenye mkutano mkuu wa APOT ulioambatana na kongamano la tano la kisayansi.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel alisema Serikali itaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya tiba ya viungo katika hospitali zote za mikoa ifikapo mwaka 2026.
Dkt. Mollel pia alitumia firsa hiyo kuwapongeza watumishi wa afya nchini wanaotoa huduma bora kwa wananchi huku akisema Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wazembe.
Pia Dkt. Mollel alikabidhi viuongo bandia kwa wahitaji 35 baada ya kufanyiwa vipimo kupitia zoezi lililoratibiwa na APOT ambapo viungo hivyo vimegharamiwa na wahisani mbalimbali ikiwemo taasisi ya SwissAbility.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA SOMA>>> APOTwafanya vipimo bure kwa wananchi
No comments: