Mashindano ya The Angeline Jimbo Cup 2024 yafana
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mashindano ya soka ya The Angeline Jimbo Cup 2024 msimu wa nane yametamatika kwa kishondo huku timu ya Kata ya Ibungilo kuibuka bingwa dhidi ya Bugogwa kwa ushindi wa goli moja kwa nunge.
Fainali ya mashindano hayo ambayo huandaliwa na mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula ilifanyika Jumamosi Oktoba 05, 2024 katika uwanja wa Sabasaba wilani Ilemela, mgeni rasmi akiwa ni Naibu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Bara, Mussa Mwakitinya.
Upande wa mshindi wa tatu ilinyakuliwa na timu ya Kata ya Kiseke baada ya kuichapa timu ya soka ya Kata ya Nyakato magoli manne kwa moja.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA
No comments: