TANESCO Mwanza waanza maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa Mwanza limezindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kufanya mdahalo wa wafanyakazi na wateja wa ndani kuhusu umuhimu wa nishati safi ya kupikia, utoaji huduma bora kwa wateja na kushiriki michezo ya kuimarisha ushirikiano (team bulding).
Maadhimisho hayo yameanza Jumatatu Oktoba 07, 2024 katika ofisi za TANESCO Mkoa Mwanza ambapo yatafikia tamati Ijumaa Oktoba 11, 2024 ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kuwatembelea wateja, kuwahudumia na kuwapa zawadi mbalimbali.
Itakumbukwa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja hufanyika duniani kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba ambapo taasisi na mashirika mbalimbali hutenga wiki hiyo kutambua mchango wa wateja kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokea maoni, ushauri na kutatua kero zao.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Idara ya Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Emmanuel Matuba akizungumza kwenye maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yaliyoanza Oktoba O7, 2024.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Afisa Masoko TANESCO Mkoa Mwanza, Prisca Kayaga akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Maafisa wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiwa kwenye mdahalo kuhusu nishati safi ya kupikia ambayo ni umeme.
Michezo ya kuimarisha ushirikiano kazini.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja/ Mteja.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja/ Mteja.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja/ Mteja.
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: