LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yaendelea kujenga Shule za Amani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema, tayari ujenzi wa shule 100 za Amali ufundi umeanza katika mikoa mbali mbali nchini.

Ujenzi wa shule hizo za Amali ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya Dkt. Samia, kuhakikisha wanafunzi wakimaliza kidato cha nne, watakuwa na uwezo wa kuajiriwa, kujiajiri na kuajiri.

Matarajio ya vijana wengi wanaosoma ni wanapomaliza kupata elimu ni kupata ajira na watoto ni wengi sana wote wanasoma kwa matarajio ya kupata ajira.

Prof. Mkenda amesema, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa maagizo kwa Wizara ya Elimu, kuweka msukumo wa mafunzo ya Amali Uhandisi yanayojikita kwenye ujuzi zaidi.

Shule hizo 100 zinazoendelea kujengwa nchini, zitaweka msukomo katika kutoa Elimu ya Michezo, Utalii, Kilimo, Uvuvi, Ufundi Umeme, Uashi na Useremala.

Ujenzi wa Shule hizo za Amali, utapewa kipaumbele katika maeneo ambayo hayana Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Wanafunzi watakaomaliza Sekondari Mafunzo ya Amali, watapata cheti cha Kidato cha Nne na cheti ya VETA na wanaweza kwenda kufanya kazi za ufundi sehemu yoyote.

Katika kuendelea kutoa fursa za mafunzo ya ujuzi, Serikali imekamilisha ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma na inatarajia kujenga vyuo vingine vinne Zanzibar na Mikoa ya Mwanza, Mtwara na Kigoma.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.