Serikali yawaboresha watanzania mazingira ya biashara nchini Congo
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Hatua hiyo inakuja baada ya nchi hizo mbili kutiliana saini mkataba wa makubaliano (MoU) wa kuboresha bandari ya kimataifa ya Kalemie na Moba pamoja na ujenzi wa bandari kavu ya Kasambondo ili kufanya shughuli za bandari kuwa za kisasa na kurahisisha usafirishaji wa mizigo kati ya DRC na Tanzania.
Katika ushirikiano huo nchi hizi mbili zimekubali pia kuboresha miundombinu ya reli inayopatikana DRC.
Makubaliano hayo yalitiwa saini kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na tayari mshauri wa mradi huo amekabidhiwa eneo hilo.
Kalemie, ni mji uliopo Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ni bandari kwenye ukingo wa magharibi wa Ziwa Tanganyika.
#KaziInaongea
No comments: