Dodoma Jiji wafika Mwanza Jiji kujifunza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeendelea kupokea Halmashauri mbalimbali nchini zinazofika kujifunza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kimkakati.
Ziara hiyo ya siku mbili imeanza Jumatatu Disemba 30,2024 ikijumuisha madiwani wa Halmashauri ya Dodoma Jiji wakiongozwa na Mstahiki Meya, Prof. Davis Mwamfupe na wataalamu mbalimbali.
"Mkiwa Mwanza mtapata fursa ya kuona na kujifunza utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo soko, meli, stendi na daraja la Busisi. Mtaona namna Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kukamilisha miradi hii iliyoachwa na mwasisi wake, hayati Dkt. John Pombe Magufuli" amesema Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha.
Miongoni mwa maeneo ambayo Halmashauri ya mbalimbali nchini hufika Halmashauri ya Jiji la Mwanza kujifunza ni namna ya kubuni na kutekeleza vyanzo vipya vya mapato na kuhusanisha miradi ya Serikali Kuu katika kuongeza mapato ya Halmashauri.
Itakumbukwa ziara hii imetanguliwa na ziara iliyofanywa na Halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara iliyofika katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya ziara ya kimafunzo.
Viongozi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakimsikiliza Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha.
Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha aliwakaribisha viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha (kushoto) akizungumza wakati wa ukaribisho wa viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha (kushoto) akizungumza wakati wa ukaribisho wa viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kulia ni Mstahiki Meya Jiji la Dodoma na kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Jiji la Dodoma.
Madiwani kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Madiwani kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Madiwani kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: