LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mariam na Hawa Wang’ara Viti Maalum Pwani – Ushindi wa Kisiasa wa Kuvutia!

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kibaha, Julai 30, 2025: Katika uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika leo katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kwamfipa – Kibaha Mjini, wagombea Hawa Mchafu Chakoma na Mariam Ibrahim wameibuka vinara katika nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani.

Jumla ya wagombea wanane (8) waliingia kwenye kinyang'anyiro hicho, ambapo kura 2,108 zilipigwa huku kura halali zikiwa ni 2,103 na kura 5 zikiwa zimeharibika. Wapiga kura waliojitokeza ni 2,095.
Katika matokeo hayo:

● Hawa Mchafu alipata kura 802

● Mariam Ibrahim alipata kura 645

● Nancy Mutalemwa kura 449

Fatuma Uwesu (71), Irene Makongoro (52), Sifa Mwaruka (44), Rehema Issa (26), na Rehema Mssemo (7).
Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi, zoezi hilo lilifanyika kwa amani na utulivu mkubwa, huku wajumbe wa CCM wakionyesha hamasa ya hali ya juu kuchagua wanawake watakaowakilisha mkoa huo bungeni.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Hawa Mchafu aliwashukuru wajumbe wa CCM kwa kuendelea kumuamini na kuahidi kuwa sauti ya wanawake na vijana wa Pwani haitazimika ndani ya Bunge.
“Nitashirikiana na kila mmoja wenu kuimarisha mshikamano, maendeleo ya kijinsia na ushiriki wa wanawake katika maamuzi ya kitaifa,” alisema Hawa Mchafu.

Kwa upande wake, Mariam Ibrahim – ambaye ni miongoni mwa nyuso mpya zilizowika kwenye kinyang’anyiro hicho – alielezea furaha yake kwa kupewa fursa ya kuwakilisha kundi la wanawake na vijana wapya katika siasa za mkoa huo.

Zoezi hilo linaonesha msukumo wa CCM wa kuendeleza usawa wa kijinsia na kutoa nafasi kwa viongozi vijana, hasa wanawake, kushiriki katika kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia Bunge.
Katika uchaguzi huo ambao umefanyika Julai 30 Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere Kwamfipa mjini Kibaha Mariam Ibrahim alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 645.

Nancy Mutalemwa alishika nafasi ya tatu baada ya kupata kura 449 akifuatiwa na Fatuma Uwesu aliyeambulia kura 71, Irene Makongoro (52), Sifa Mwaruka (44), Rehema Issa(26) na Rehema Mssemo (7).

Kura halali katika uchaguzi huo zilikuwa 2108, zilizopigwa ni 2095 na zilizoharibika ni tano.

No comments:

Powered by Blogger.