LIVE STREAM ADS

Header Ads

TCCIA yaahidi kuboresha zaidi Maonesho ya Biashara Afrika Mashariki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) imeahidi kufanya maboresho na kuyatangaza zaidi Maonesho ya Biashara Afrika Mashariki, ili kuyapa hadhi zaidi na kuongeza wigo wa washiriki wa maonesho hayo.

Rais wa Chemba hiyo, Vicent Minja aliyasema hayo Jumanne Agosti 02, 2025 wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 20 ya Afrika Mashariki yanayofanyika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Minja alisema tayari TCCIA imeanza mikakati ya kuyafanya maonesho hayo kuvutia washiriki wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi na kwamba changamoto kama eneo maalumu la kufanyia maonesho itatafutiwa ufumbuzi.

Akifungua maonesho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda alisema Mwanza ni eneo linalofikika kwa urahisi katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki hivyo Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya ikiwemo usafiri wa majini na nchi kavu hatua itakayoongeza ushiriki mkubwa wa maonesho hayo.

Maonesho ya 20 ya Biashara Afrika Mashariki yalianza Agosti 29, 2025 na yatafikia tamati Septemba 07, 2025 yakiwa na kaulimbiu isemayo "Biashara Kijani, Uchumi Mzunguko, Maisha Endelevu".
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda (kushoto) akiwasili uwanja wa Nyamagana kufungua Maonesho ya 20 ya Afrika Mashariki ambayo huandaliwa na TCCIA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda akiwa kwenye banda la TBS kwenye maonesho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda akiwa kwenye banda la TBS kwenye maonesho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda akiwa kwenye banda la Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda akikabidhi tuzo na vyeti kwa washiriki bora wa maonesho hayo. Anayepokea tuzo ni mwakilishi kutoka TANESCO.
Rais wa TCCIA, Vicent Minja (wa pili kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene (wa pili kulia).
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.