LIVE STREAM ADS

Header Ads

ASKOFU MKUU MSTAAFU KANISA LA AIC KUZINDUA VITABU MUHIMU

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la “African Inland Church Tanzania” (AICT), Dkt. Methuselah Paul Nyagwasa (94), anatarajia kuzindua vitabu viwili vyenye maudhui mbalimbali ikiwemo historia ya kanisa na maisha yake.

Akizungumza na wanahabari Jumanne Septemba 03, 2025 jijini Mwanza, Dkt. Nyagwasa ambaye ni Askofu wa pili wa kanisa hilo la AIC, amevitaja vitabu hivyo kuwa ni “Kanisa Langu AIC, Maisha Yangu” na “Mifano Hai”.

Dkt. Nyagwasa amesema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Jumamosi Septemba 06, 2025 katika eneo la Kwa Kishimba Rock Beach jijini Mwanza kuanzia majira ya saa nne asubuhi ukiambatana na sherehe ya miaka 94 tangu kuzaliwa Septemba 05, 1931.

Aidha Dkt. Nyagwasa amemshukuru Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko kwa kumpa msukumo wa kuandika vitabu hivyo pamoja na mwandishi Denis Mpagaze kwa kumsaidia kufanikisha uandishi huo.
Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la AICT, Dkt. Methuselah Paul Nyagwasa (94), akionyesha vitabu vyake. Kushoto ni kitabu cha Mifano hai na kulia ni kitabu cha Kanisa Langu AIC, Maisha Yangu.
Uzinduzi unatarajiwa kufanyika Jumamosi Septemba 06, 2025 katika eneo la Kwa Kishimba Rock Beach jijini Mwanza kuanzia majira ya saa nne asubuhi ukiambatana na sherehe ya miaka 94 tangu kuzaliwa Septemba 05, 1931.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.