HATMA YA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA KAMANDA BARLOW BADO KITENDAWILI.
![]() |
Aliekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza-Barlow |
Kesi
ya Mauwaji ya aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Riberatus
Barlow, imeendelea kusomwa katika Mahaka ya Hakimu Mkazi Mkoani Mwanza.
Kesi hiyo ambayo inawakabiri
watuhumiwa
saba inaendelea kupigwa tarehe kutokana na ushahidi wake
kutokamilika mpaka sasa.
Watuhumiwa hao ni Muganyizi Maicco Peter (30) Mkazi wa Nyakabungo Mkoani
Mwanza, Chacha Wekena Mwita (50) Mkazi wa Gongo la Mboto Jijini Dar es salaam,
Magige Mwita Marwa (48) Mkazi wa Bugarika Mkoani Mwanza.
Wengine ni Mganzi Edward (22) Mkazi wa Tandika Jijini Dar es
salaam, Bhoke Marwa Mwita (42) Mkazi wa Mombasa Ukonga, Andallah Petro (32)
Mkazi wa Mji Mwema Mkoani Mwanza na Abdulhaman Ismail Athman (28) Mkazi wa
Mkudi Mkoani Mwanza.
Hakimu Mkazi Angelous Rumishaba, alieleza kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa
na kesi namba 30 ya mwaka 2012 ya mauaji kinyume na kifungu cha sheria 196 na 197 ya sheria ya kanuni za
adhabu,sura ya 16 iliyofanyiwa marejesho mwaka 2002.
Alieleza kwamba washitakiwa hao walitenga kosa hilo la mauwaji
usiku wa kuamkia Oktoba 13 mwaka 2012,katika eneo la kitangiri minazi mitatu
wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Kamanda Barlow aliuawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi,
mwaka 2012, majira ya saa nane usiku kwa kupigwa risasi shingoni, wakati
akirejea nyumbani kwake akitoka katika kikao cha harusi ya binamu yake.
Kesi hiyo ilisomwa jumanne wiki hii na imeahirishwa tena hadi Septemba nne
mwaka huu itakaposomwa tena.
Na Prisca Japhes: Mtanzania Media-Mwanza.
No comments: