 |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata. |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata amewajia juu wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA
ambao wamesusia vikao vya bunge maalumu la Katiba kwa madai kwamba wameingilia majukumu ambayo yako inje ya Uwezo wao.
Matata alitoa kauli hiyo jana wakati akiahirisha kikao cha baraza la madiwani wa Manispaa hiyo, ambacho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo uliopo Buswelu Wilayani Ilemela.
Alisema kuwa kitendo cha UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba kinaashiria uoga na wasiwasi juu ya hoja zao, jambo ambalo si jema kwa kuwa linaweza kutia doa mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba mpya hapa nchini.
Aidha Matata aliwashauri UKAWA kurejea Bungeni hata kama watakuwa na hofu juu ya Hoja zao kushindwa, kwa kuwa Wajumbe wa Bunge hilo sio waamuzi wa Mwisho wa Kupitishisha Katiba Mpya, bali wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho hivyo waondoe wasiwasi waliowao.
 |
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Justin Lukaza (Kushoto) akifuatiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata (Kulia). |
Uchaguzi wa Kumpata Naibu Meya wa Manispaa ya
Ilemela Mkoani Mwanza ulifanyika jana huku kukishuhudiwa Mgomea Mmoja
kutoka Chama cha Mapinduzi CCM akisimama peke yake,
ambapo vyama vingine vya siasa havikuweza kusimamisha mgombea wake.
Katika
Uchaguzi huo, Dede Swila Dede ambae ni Diwani wa Kata ya Bugogwa (CCM)
aliweza kutetea nafasi ya Unaibu Meya katika Manispaa hiyo baada ya
kupigiwa Kura ya Ndiyo/ Hapana. Alichaguliwa kwa Kura Sita za Ndyo, huku
Kura Mbili zikisema Hapana.Pia wenyeviti wa kamati za maendeleo katika
manispaa hiyo waliweza kuchaguliwa.
Kwa mjibu wa
Sheria na kanuni ni kwamba Naibu Meya sanjari na wenyeviti wa kamati za
maendeleo huchaguliwa kila baada ya kipindi cha Mwaka Mmoja na Dede
ametetea nafasi yake ya Naibu Meya kwa awamu zote tatu tangu Manispaa ya
Ilemela ianze kujitegemea baada ya kugawanyika kutoka katika
Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
 |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata (Kushoto) akiwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Dede Swila Dede (Kulia). |
Kitendo cha Uchaguzi huo kufanyika huku kukiwa na Mgombea Mmoja wa Chama cha Mapinduzi CCM kilipelekea Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza Highness Kiwia (Chadema) kutoa Malalamiko yake kwa Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo huku ikielezwa kuwa uchaguzi huo usingeweza kuahirishwa kwa kuwa vyamba vyote vilipewa taarifa ya kusimamisha mgombea wake tangu tarehe 29.07.2014 lakini vyama hivyo havikuweza kumsimamisha mgombea wake.
 |
Mwanasheria wa Manispaa ya Ilemela (Menye shati jeupe) akihesabu kura zilizopigwa jana katika uchaguzi wa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. |
 |
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. |
 |
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. |
 |
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. |
 |
Taswira ya Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. |
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.
No comments: