WAKAZI WA MBUGANI JIJINI MWANZA WATAKIWA KUTOTEGEMEA MISAADA.
Wakazi
wa kata ya Mbugani Jijini Mwanza wametakiwa kutotegemea misaada
kutoka serikalini, ili kukuza uchumi na kuboresha rasilimali
zilizopo kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza ofisini kwake
Mwenyekiti
wa mtaa wa Mabatini Kaskazini kata ya Mbugani Ntobi Boniphas alisema kuwa
wakazi wa maeneo hayo wanatakiwa kujituma katika shughuli mbalimbali ili kuleta
maendeleo katika kata zao.
Alieleza kuwa zipo shughuli nyingi
ambazo zinapaswa kufanywa na jamii husika bila kutegemea nguvu ya serikali wala
msaada wowote hususani katika utengezaji wa barabara za mitaa, ujenzi wa
maabara na miradi mingine ya kimaendeeleo.
“ Tunatatizo la barabara kwa muda
mrefu hali inayosababisha wananchi wakati wa mvua kushindwa kutoka majumbani
kwenda katika shughuli zao za kila siku wakati uwezo wa kurekebisha barabara
hizo tunao sisi kama jamii.”Alisema Boniphas.
Mwenyekiti huyo Pia katika
kuhakikisha jamii inahusika kwa kila hali kuchangia maendeleo, alisema uongozi
wa eneo hilo hutumia mikutano ya hadhara kuwahamasisha wananchi kujiletea
maendeleo na kuzungumzia changamoto mbalimbali na jinsi ya kukabiliana nazo
kama vile elimu, afya na miundombinu ya kata.
Pamoja na kuwepo na juhudi hizo za
kuleta maendeleo ndani ya kata,Boniphas alieleza kwamba hali ya ulinzi na
usalama katika eneo hilo inaridhisha kutokana na kuwepo na ushirikiano na
polisi jamii licha ya kuwa kila mwananchi anajukumu la kulinda amani
katika eneo lake analoishi.
Hata hivyo amewataka wageni
wanaoingia mtaani hapo kudumisha amani pia ushirikiano wanaoukuta ili kupunguza
matukio ya kihalifu ambayo hapo awali yalikuwa mengi katika baadhi ya
mitaa.
Na Prisca Japhes
No comments: