LIVE STREAM ADS

Header Ads

AZAM FC WAPOKELEWA KIGAIDI CHINI SUDAN.

WAPEWA ‘GARI LA MKAA’ , WACHEZAJI WAPIGISHWA KWATA UWANJA WA NDEGE.

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam FC wamepata mapokezi ya ‘kigaidi’ mjini Khartoum, Sudan baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya mchezo na wenyeji, El Merreikh. Kwanza, walipotua Uwanja wa Ndege, wachezaji na msafara mzima walianza kufanyiwa vitimbi na watu wa Idara ya Uhamiaji katika kupatiwa visa za kuingia nchini humo. 

Baada ya kuufuzu mtihani huo, walikutana na visa zaidi walipotoka nje ya Uwanja wa Ndege, kufokewa na watu waliokwenda kuwapokea, kabla ya kwenda kuwapakia katika basi bovu na baya aina ya Coaster. 20152/25/2015 AZAM FC WAPOKEWA ‘KIGAIDI’ SUDAN, WAPEWA ‘GARI LA MKAA’, 

WACHEZAJI WAPIGISHWA KWATA UWANJA WA NDEGE ­ BIN ZUBEIRY http://bongostaz.blogspot.com/2015/02/azam­fc­wapokewa­kigaidi­sudan­wapewa.html 3/11 Basi aina ya Coaster ambalo wamepewa Azam FC Sudan Pamoja na hayo, Azam FC kwa kuwa walijua watakutana na hali kama hiyo, hawakuonekana kustaajabu, badala yake kuvumilia yote. 

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Khartoum kwamba wamefanyiwa mambo ambayo kwa ujumla si ya kuanamichezo. “Tunarekodi kila kitu na tutatuma CAF (Shirikisho la Soka Afrika). 

Sisi hatuna wasiwasi nao, kwa sababu tunawajua,”amesema. Kikosi cha wachezaji 23 wa Azam kimewasili Khartoum tayari kwa mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa wiki. 

Azam FC inahitaji hata sare au kutofungwa kwa wastani wa zaidi ya bao 1­0 ili kusoga mbele kwenye michuano hiyo, baada ya awali kushinda 2­0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wiki iliyopita.
Kwa Hisani ya Bin Zubery.

No comments:

Powered by Blogger.