HAPPY BIRTH DAY GB AMBAE NI C.E.O WA BINAGI MEDIA GROUP NA STAFF WA METRO FM.
![]() |
George Marwa Binagi-GB Pazzo. |
Ilikuwa
ni February 26 Miaka kadhaa iliyopita, Mtoto George Marwa Binagi, GB Pazzo kama
ninavyojulikana zaidi kwa hivi sasa niliweza kuzaliwa ambapo kuzaliwa kwangu
kulitokana na Ushirikiano mzuri kati ya Wazazi wangu wapendwa The Late Mzee
Daniel Marwa Binagi pamoja na Leah Daniel Binagi.
Hakika ni jambo jema kuona kwamba pamoja na changamoto zote katika
uso wa dunia hii, bado Mola anazidi kunitazama kwa jicho la pekee na hatimae
leo alhamisi February 26, 2015 nimeongeza idadi ya miaka tangu kuzaliwa kwangu.
Japo bado safari ni ndefu lakini mimi nasema kwamba haikuwa kazi
rahisi hadi kufikia hatua niliyoifikia hivi sasa katika kuelekea kwenye
mafanikio yangu, bali ni kwa rehema na Uweza wa Roho Mtakatifu.
Hakika sitawasahau ndugu, jamaa na marafiki wote ambao kwa namna moja
ama nyingine waliweza kufanyika msaada mkubwa kwangu na hatimae hii leo
nimefika hapa nilipo. Yapo mengi ambayo yametendeka. Mengi mazuri na machache
mabaya. Sina neno la kusema zaidi ya MNISAMEHE PALE NILIPOWAKWAZA. Kwa upande
wangu moyo wangu ni mweupe na hakuna hata mmoja nilie na kinyongo nae. Hakika
Mwenyezi Mungu azidi kutuongoza vyema.
Yapo mengi sana ya kusema ila najua nikiyasema yataiondoa furaha niliyonayo
siku ya leo, hivyo sina budi kuyaacha. Nikiwa Mtangazaji na Mwandishi wa Habari
ninaefanya kazi na 99.4 Radio Metro Fm, Mwanza na C.E.O wa Binagi Media Group,
nina imani kwamba siku zote jamii inayonizunguka itaendelea kunufaika na kazi zangu
huku nikilenga zaidi kuchochea uelewa na mabadiliko ya kimaendeleo kwa kila
mmoja.
NIMEJIFUNZA KWAMBA HAKUNA MAFANIKIO BILA CHANGAMOTO HIVYO TUSIKATE
TAMAA PALE TUNAPOKUMBANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI. JAMBO PEKEE NINALOWEZA
KUTAMATISHA NALO NI KWAMBA “MTU AKIWA NDANI YA KRISTO, AMEKUWA KIUMBE KIPYA, YA
KALE YOTE YAMEPITA, TAZAMA YAMEKUWA MAPYA”. 2 WAKORINTHO 5:17.
"HAPPY BIRTH DAY TO MYSELF".
No comments: