LIVE STREAM ADS

Header Ads

HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA YASAINI MIKATABA YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 800 KWA AJILI YA UKARABATI WA BARABARA ZAKE.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akijionea kipande cha barabara kilichoharibika katika Mtaa wa Kasese Kata ya Mkolani Jijini Mwanza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya barabara Jijini Mwanza ambayo iko katika ukarabati na matengenezo mbalimbali.
Na:George GB Pazzo
Katika Kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi, Halmashauri ya Jiji la Mwanza imesaini Mikataba tisa na Wakandarasi  mbalimbali ikiwa na thamani yenye zaidi ya Shilingi Milioni 800, kwa ajili ya kufanya matengenezo na ukarabati wa barabara mbalimbali katika Kata zote zilizopo Jijini Mwanza.

Akizungumza jana wakati wa kuwakabidhi Wakandarasi hao Mikataba hiyo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula aliwataka Wakandarasi waliopewa mikataba hiyo kutekeleza kazi waliyopewa kwa ufasaha zaidi ikiwa ni pamoja na kuzingatia ubora na muda uliopangwa.

Mabula alisema kuwa takribani Kilomita 19.5 za barabara katika maeneo tofauti tofauti ya Jijini la Mwanza zinatarajiwa kufanyiwa ukarabati wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja barabara ambazo zitarekebishwa kwa kiwango cha Lami na nyingine katika kiwango cha Moramu sanjari na zile ambazo pia zitachongwa na kuwekewa makaravati.

Alisema kuwa mbali na ukarabati huo pia yupo Mkandarasi Mmoa ambae amepewa jukumu la kuhakikisha kuwa anaweka alama za barabarani katika barabara zote zilizo katikati ya Jiji la Mwanza sanjari na Mkandarasi mwingine ambae atakuwa na jukumu la kuzibua mitaro katikati ya Jiji la Mwanza ambayo imeziba na hivyo kuleta adha kubwa Jijini Mwanza katika kipindi cha mvua.

Miongoni mwa barabara zitakazofanyiwa ukarabati ni pamoja na Barabara ya Ushirika eneo la Kemondo, Barabara ya Tambukareli, Barabara ya Nyegezi Stand hadi Mkolani Sekondary, Barabara ya Nyang’ing'i Mkolani pamoja na Barabara ya Mwananchi hadi Alliance ambapo baadhi ya barabara ukarabati huo utaenda sawa na ujenzi wa mitaro na makaravati.

Baada ya Wakandarasi hao kukabidhiwa Mikataba yao, Meya Mabula alifanya ziara katika maeneo yao ya kazi ambapo kwa barabara zinazotengenezwa kwa kiwango cha Moramu alisema kuwa halmashauri ya Jiji la Mwanza imeona ni vyema kufanya ukarabati wa aina hiyo kulingana na Uwezo wake wa Kifedha ambao hauwezi kukidhi gharama za barabara zote kufanyiwa ukarabati katika kiwango cha lami.

Nao baadhi ya waendesha pikipiki Jijini Mwanza ambao pia ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa barabara katika shughuli zao, waliishauri halmashauri ya Jiji la Mwanza kuongeza juhudi zaidi katika kufanya ukarabati wa barabara zake ili kuwawezesha kufanya shughuli zao vyema huku wakiwahimiza wakandarasi waliopewa kandarasi za kufanya ukarabati Jijini Mwanza kuzingatia ubora na viwango katika kazi waliyopewa.

Kwa upande wake Mkelewe Masaru Tungaraza ambae ni Mhandisi wa barabara Jijini Mwanza alibainisha kwamba katika kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara, changamoto kubwa inayolikabili Jiji la Mwanza ni ufinyu wa bajeti hali ambayo imekuwa ikisababisha barabara nyingi kutorekebishwa kwa ubora unaohitajika huku changamoto nyingine ikiwa ni pamoja na ujenzi holela ambao umekuwa ukisababisha mvutano na wananchi katika kuwahamisha wananchi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula (katikati) akikagua barabara ya Nyang'ing'i Mkolani wakati wa ziara yake siku ya jana.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akikagua mwenendo wa kazi katika barabara ya Nyegezi Stand kwenda Mkolani Sekondari.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akikagua mwenendo wa kazi katika barabara ya Nyegezi Stand kwenda Mkolani Sekondari.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akikagua ujenzi wa karavati katika daraja la Mahina.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akikagua zoezi la kuzibua mitaro katika barabara ya Uhuru Jijini Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula (Kulia) akisaini daftari la wageni baada ya kufika katika barabara ya Mwananchi hadi Alliance kwa ajili kujionea ukarabati katika barabara hiyo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akimsikiliza mmoja wa wananchi ambae ni mtumiaji wad daraja la Mahina ambalo liko katika ukarabati wa karavati.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akikagua ujenzi wa karavati katika daraja la Mahina (mwenye miwani) akiwa katika ukaguzi wa barabara eneo la Tambukareli.
Baadhi ya Wakandarasi wakiwa pamoja na baadhi ya Watendaji mbalimbali kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula (Kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa mkandarasi anaefanya ukarabati katika barabara ya Mwananchi hadi Alliance.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akizungumza na wanahabari wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara Jijini Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula (nyuma) akiwa na Nyamisango Stephen ambae ni Muuguzi Mkuu wa Zahanati ya Tambukareli wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara ya Tambukareli siku ya jana.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akionyeshwa mipaka ya eneo la Zahanati ya Tambukareli na Nyamisango Stephen ambae ni Muuguzi Mkuu wa Zahanati hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara ya Tambukareli siku ya jana.
Hongereni wananchi wa Tambukareli kwa Zahanati hii.
Adha waipatayo watumiaji wa barabara ya Ushirika eneo la Kemondo itaomalizwa hivi karibuni baada ya halmashauri ya Jiji la Mwanza kuingia mkataba na mkandarasi kwa ajili ya kuifanyia matengenezo kwa kiwango cha lami.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akijionea jinsi barabara ya Ushirika Kemondo ilivyoharibika. Barabara hii ni miongoni mwa barabara zitakazokarabatiwa.
Waendesha bodaboda eneo la Msikitini Mkolani Wakishow love na Binagi Media Group baada ya Mazungumzo.
GB (wa kwanza kulia) CEO wa Binagi Media Group akiwa na waandishi wengine katika ziara ya Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula.
GB (wa kwanza kulia) CEO wa Binagi Media Group akiwa na waandishi wengine katika ziara ya Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akizungumza ofisini kwake jana kabla ya kuwakabidhi mikataba wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara Jijini Mwanza.
Wakandarasi wakiwa katika ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza kwa ajili ya kupokea Mikata yao ya kazi.
Wakandarasi wakiwa katika ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza kwa ajili ya kupokea Mikata yao ya kazi (Waliokaa). Waliosimama ni wanahabari.
Wakandarasi wakiwa katika ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza kwa ajili ya kupokea Mikata yao ya kazi (Waliokaa). Waliosimama ni wanahabari.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula (Kushoto) akiwakabidhi mikataba wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara Jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.