WANAOFADHIRI UTEKAJI WA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI WATAJWA.
Kufuatia
Vitendo vya Utekaji na Maua kwa Watu wenye Ulemavu wa ngozi kuendelea kushamiri
hapa nchini, Watu wanaodhaniwa kufadhiri vitendo hivyo wamefichuliwa ambapo
Serikali imetakiwa kuwachulia hatua mara moja badala ya kuishia kusema hakuna
Ushahidi wa Kutosha.
Akizungumza hivi Karibuni Jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Shirika la
Kutetea haki za Watu wenye Ulemavu wa Ngozi Under The Same Sun lenye Makao yake
Makuu nchini Canada Peter Ashi, alisema kuwa viungo vya watu wenye ulemavu wa
ngozi vinauzwa kwa thamani kubwa hivyo wananchi wa kawaida hawawezi kumudu
kuvinunua.
Kutokana na hali hiyo Ash aliwatupia lawama Wanasiasa kwa kuhusika
moja kwa moja na vitendo hivyo vya kufadhiri Utekaji na Mauaji ya watu wenye
Ulemavu wa ngozi hapa nchinini huku akiongeza kuwa mbali na baadhi ya watu waliowahi
kukamatwa kwa kujihusisha na utekaji na mauaji ya Watu wenye ulemavu wa ngozi pia
ongezeko la vitendo hivyo katika kipindi cha chaguzi hapa nchini vinaashiria
kwamba baadhi ya wanasiasa wanajihusisha moja kwa moja na ufadhiri wa vitendo
hivyo vya utekaji na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Ash aliyazungumza hayo huku akilaani tukio lililotokea disemba 27 mwaka
jana ambapo mtoto ambae ni mlemavu wa ngozi Pendo Emmanuel (4) mkazi wa Kijiji
cha ndami Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza kutekwa nyumbani kwao akiwa na wazazi
wake ambapo mpaka sasa mtoto huyo hajaweza kupatikana licha ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Magesa Mulongo kutoa siku tano mtoto huyo awe amepatikana aidha akiwa
hai ama mfu.
Wakati tukio hilo likiwaaacha watu wenye ulemavu wa ngozi wasijue
la kufanya kutokana na maisha yao kuwa katika hali ya wasiwasi, mtoto Yohana
Bahati (1) mkazi wa Kijiji cha Ilelema Wilaya ya Chato Mkoani Geita juzi
January 15 majira ya saa mbili usiku pia ametekwa akiwa mikononi mwa mama yake
mzazi huku watekaji hao wakimjeruhi mama yake Esther Bahati (30) wakati
akipambana katika kumuokoa mwanae. Mama huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa
Bugando na hali yake inaelewa kuwa mbaya kiasi cha kumfanya ashindwe kuongea
baada ya kujeruhiwa kwa mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Bado juhudi za jeshi la polisi hapa nchini katika kuwalinda watu
wenye ulemavu wa ngozi hazijaweza kuzaa matunda ambapo juhudi zaidi zinahimizwa
kuongezeka huku ndugu, jamaa na marafiki wakitakiwa kuongeza ushirikiano wao
katika kuyanusuru maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi kutokana na
unyanyasaji, utekaji na hata mauaji.
Sanjari na nayo, pia onyo lililotolewa hivi karibu na Serikali juu
ya kuwapiga marufuku waganga wa kienyeji kujihusisha na vitendo vya ramli
limetakiwa kutekelezwa ipasavyo kutokana na shuhuda mbalimbali kuonyesha kwamba
matukio mengi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi huchochewa vitendo vya
lamri ambavyo vimekuwa vikifanywa na waganga wa kienyeji kwa kuwatabiria wateja
wao kupeleka viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa minajiri ya kuwapatia
utajiri ama kuwafanikishia masuala yao mbalimbali jambo ambalo si sahihi.
Wakizungumza na Binagi Media Binagi baadhi ya watu wenye ulemavu
wa ngozi pamoja na ndugu, jamaa na rafiki zao wameishauri Serikali kutenga
maeneo maalumu hapa nchini kwa lengo la kuwaweka watu wenye ulemavu wa ngozi
pamoja ikiwa ni pamoja na kupatiwa huduma muhimu kama vile elimu, afya sanjari
na ulinzi imara katika maeneo hayo.
Na: George Binagi-GB Pazzo
No comments: