MABULA: NAOMBENI RIDHAA YENU NIWAWAKILISHE.
Na:Binagi Media Group
Aliekuwa diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula amesema kuwa Wananchi ndio watakao Mpandisha ama kumshusha katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
Mabula ambae ni miongoni mwa watia nia 20 waliochukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ili kupata nafasi ya kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Nyamagana, alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na Radio ya Metro.
"Nimejitahidi kuwatumikia wananchi tangu nilipochaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Mkolani mwaka 2010 na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza tangu Mwaka 2012. Mabadiliko yote haya unayoyaona hivi sasa ni kutokana na jitihada zangu, hivyo mimi nasema katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa mwaka huu, Wananchi ndio watakaoamua ikiwa ni kunipandisha au kunishusha". Alisema Mabula.
Aidha Mabula anawahimiza WanaCCM kutofanya makosa Agosti Mosi Mwaka huu katika kura za kumchagua mgombea atakaeipeperusha bendera ya chama hicho katika Jimbo la Nyamagana akiomba ridhaa yao ili awawakilishe wananchi wote kwa ujumla.

No comments: