LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATIA NIA CCM KATA YA NYAMANORO WILAYANIM ILEMELA WATIA FOLA KWA TAMBWE.

Na:Judith Ferdinand na Neema Emmanuel
Makada Sita wa Chama cha Mapinduzi CCM wamejitokeza kuwania nafasi ya kugombea udiwani katika Kata ya Nyamanoro Wilayani Ilemela, ambapo kila mmoja ametoa ahadi kwa wanachama na wananchi ya kuleta maendeleo ikiwa atapata ridhaa ya kuchaguliwa.

Miongoni mwa makada hao ni Abdulrahaman Kange, George Maganiko, Yaqub Muro, Barnabas Luhega, Amini Fataki huku Jaruph Kulindwa akijitoa dakika za mwisho katika kinyang’anyiro hicho baada ya kuchukua fomu.

Wakizungumza na Binagi Media Group kwa nyakati tofauti, wagombea hao kila mmoja alikuwa na yake ya kujinadi nayo.

Kange alisema kuwa endapo kama ataibuka mshindi ndani ya chama katika kura za maoni zinazotarajiwa kupigwa Agousti 1 mwaka huu na hatimaye kushinda katika uchaguzi mkuu, atahakikisha anashirikiana na wananchi ili kuleta maendeleo na kutatua changamoto zinazoikabili kata hiyo ikiwemo maji, miundo mbinu, elimu, afya, ajira na michezo.

Kwa upande wake Maganiko aliwaomba wanaCCM wamtume kwani anajua changamoto za kata hiyo na yupo tayari kuzitatua kwa kushirikiana na wananchi pamoja na kusimamia ilani ya chama, pia alisema kuwa anao uwezo wa kuikomboa Kata hiyo kutoka mikononi mwa wapinzani.

Naye Muro alisema endapo kama atapatiwa nafasi na chama ya kupeperusha bendera yake kwa ngazi ya udiwani na kushinda katika uchaguzi mkuu mwaka huu atahakikisha anatatua kero zinazokabili wananchi wa kata hiyo kwa kushirikiana nao, kwani umefika muda wa kuwatumikia.

Hata hivyo kwa upande wake Fataki alisema kuwa kutokana na adha wanazopata wakazi wa kata hiyo baada ya wapinzani kushidwa kutatua kero zinazowakabiri ikiwemo maji, miundo mbinu, elimu, afya na sehamu ya kutupiua taka, atahakikisha anazitatua kwa kushirikiana na wananchi endapo kama wanaCCM watampatia ridhaa hiyo kwa kumpigia kura za ndiyo ndani ya chama na katika uchaguzi mkuu.

Aidha Luhega alisema kuwa matumaini yake wanaCCMwatachagua kiongozi bora asiyetoa wala kupokea rushwa, hivyo wakimchagua yeye hawatajuta kwani atahakikisha anayasemea matatizo na changamoto zinazowakabili wananchi wa kata hiyo ikiwemo maji, barabara, elimu na hata kupigania haki ya wafanyabiashara ndogondgo wa maeneo hayo wanao nyang’anywa bidhaa zao na kwa mgambo kwa kisingizio cha usafi. 

Kadhalika Kulindwa alisema alikuwa na nia ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi wa Kata hiyo lakini aliamua kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho kutokana na mizengwe iliyopo ndani ya chama chama chake.

No comments:

Powered by Blogger.