LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU YA WANAHABARI JIJINI MWANZA YAANZA VIBAYA KATIKA MICHUANO YA MEYA CUP 2015.

Na:Oscar Mihayo
Timu ya Wanahabari Mkoani Mwanza imeanza vibaya katika mashindano ya Meya Cup, baada ya kutandikwa mabao 2-1 na timu ya machinga Fc katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Kona ya Nyegezi.

Mchezo huo wa kwanza kwa Wanahabari ulikuwa wa vuta ni kuvute kufuatia timu zote kujiandaa vya kutosha huku refarii wa mchezo huo akionekana kushindwa kuumudu mchezo huo.

Wanahabari ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa mfungaji wake Michael Joram katika kipindi cha kwanza kabla ya  Machinga fc kuzindika na kusawazisha kupitia kwa Mwinyi Akida dakika ya 48 kabla ya kuongeza bao la pili na la ushindi dakika ya 68 ya mchezo.

Mara baaada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Wanahabari Almas Moshi alisema kuwa maamuzi ya mwamuzi wa mchezuo huo hakuwa sahihi kwa kutoa maamuzi yenye utata jambo lililopelekea timu yake kupoteza mchezo huo wa kwanza na wa muhimu kwa timu yake.

Kwa upande wa Kocha wa Machinga Fc Aron George alisema kuwa ushindi wao wa kwanza hawakubatisha huku akitoa salamu kwa timu shiriki zote kujiandaa kunyolewa kwani wamejiandaa vya kutosha.

Bonyeza HAPA Kujua Zaidi Kuhusu Michuano Hiyo.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi Kuhusu Machinga United

No comments:

Powered by Blogger.