LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA WALIMU MKOA MKOANI MWANZA CHAICHARUKIA SERIKALI.

Na:Judith Ferdinand
Chama cha Walimu Mkoa wa Mwanza (CWT) kimesema kuwa takribani waalimu zaidi ya 2000 mkoani  Mwanza wanaidai serikali malimbikizo ya mishahara pamoja na gharama za upandishwaji wa madaraja huku zaidi ya waalimu 3000 wakiwa wanadai pesa za likizo na matibabu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CWT Mkoani Mwanza Sibora Kisheri alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuunga mkono kauli ya Rais wa CWT Taifa Gratian Mkoba aliyoitoa agousti  19 mwaka huu Jijini Dar es salaam.

"CWT inaunga mkono kauli ya rais wake aliyoitoa katika mkutano mkuu wa CWT, uliofanyika Ngurudoto mkoani Arusha ya kuitaka serikali kulipa madeni inayodaiwa na waalimu kabla ya mwezi septemba ikizingatiwa kuwa Rais Kikwete aliahidi kulipa madeni hayo kabla ya uchaguzi mkuu". Alisema Kisheri na kuongeza;

“Mwanza tupo tayari kupokea maelekezo kutoka CWT makao makuu na kuyaunga mkono na tunataka haki yetu ilipwe kwa wakati, maana walimu tunaathirika ikizingatiwa tunafanya kazi katika mazingira magumu".

Naye Katibu wa CWT mkoa wa Mwanza Said Mselem aliiomba serikali kuwahusisha waalimu wakati wa upangaji wa bajeti ya elimu kwa kuwa wakati wa kupitisha bajeti hiyo waalimu wamekuwa hawahusishwi na hivyo kuwawia vigumu katika ufuatiliaji wa stahiki zao.

Mselem  alisisitiza kuwa kwa sasa CWT Mkoa wa Mwanza haitakubali serikali serikali ifanye uhamisho wa mwalimu yeyote kutoka Mwanza kwenda eneo tofauti kabla ya kulipwa gharama zake za uhamisho.

No comments:

Powered by Blogger.