LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDERICK SUMAYE AJIUNGA NA UKAWA. SABABU ZIKO HAPA.

Waziri Mkuu Mstaafu Fredirick Sumaye ametangaza rasmi Msimamo wake wa kujiunga na Upinzani akitokea Chama Tawala, Chama cha Mapinduzi CCM. Ametangaza hii leo katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam. Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi wa Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa.
Na:George GB Pazzo
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania katika Serikali ya awamu ya tatu Mhe.Frederick Sumaye ametangaza rasmi kujiunga na Upinzani.

Sumaye ametangaza kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA dakika chache zilizopita, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Dar es salaam.

Katika Mkutano huo ambao umehudhuriwa na Viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA, Sumaye amebainisha kuwa amejitoa CCM baada ya kutoridhishwa na mfumo wake wa uongozi ikiwemo namna kilivyowapata wagombea watakaoipeperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

"Mimi nimejitoa CCM na nimejiunga na Ukawa. Chama gani ndani ya Ukawa tutajua mbele ya Safari". Amesema Sumaye wakati akitangaza kung'atuka ndani ya CCM na kuongeza kuwa amejitoa CCM ili kusaidiana na Wanaukawa kwa ajili ya kuwaletea watanzania mabadiliko wanayoyataka.

Taarifa za Sumaye kujitoa CCM zinajiri ikiwa ni takribani juma moja baada ya aliekuwa Meneja Kampeni wake John Mlema kukana taarifa zilizokuwa zimezagaa kuwa Sumaye amejiunga na Ukawa. SOMA HAPA Taarifa hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.