LIVE STREAM ADS

Header Ads

+AUDIO: CHADEMA YAISHAURI SERIKALI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA JIJINI MWANZA.

Kushoto ni Katibu Mkuu Taifa BAWACHA, Grace Tendega na Kulia ni Mbunge Viti Maalumu Mkoani Mwanza (Chadema) Susan Masele.
Serikali imeshauriwa kuboresha huduma za Afya katika Vituo vya Afya na Zahanati Jijini Mwanza, ili kupungumza msongamano wa Wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure.

Ushauri huo ulitolewa jumamosi iliyopita na Grace Tendega ambae ni Katibu Mkuu Taifa wa Baraza la Wanawake Chadema BAWACHA, alipoungana na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) Susan Masele na kufanya ziara ya kuwatembelea wagonjwa katika hospitali hiyo, kabla ya kufanya uzinduzi wa ofisi ya Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) iliyopo Ghana Green View Jimboni Ilemela.

Tendega alisema kuwa ziara hiyo imebaini changamoto kadhaa katika Hospitali ya Sekour Toure ambazo ni pamoja na mrundikano wa wagonjwa hususani katika wodi ya kujifunguliavakina mama wajawazito, ambapo ameshauri kuwa serikali ikiboresha huduma za afya katika vituo vya Afya na Zahanati, msongamano huo utapungua hospitalini hapo.

Pamoja na mambo mengine, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) Susan Masele, alisema ni vyema serikali ikaongeza bajeti ya wizara ya afya na kuisimamia ili kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchini ambapo pia ameahidi kuwasilisha mapendekezo yake bungeni ili serikali kuweza kutatua changamoto za kiafya Mkoani Mwanza.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sekour Toure Dkt.Onesmo Rwakyendela, alikubaliana na hoja ya kuboresha huduma za afya katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Mwanza, hususani huduma za uzazi.

Hata hivyo baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mwanza walieleza kuwa wanakiri kuwemo kwa changamoto za upatikanaji wa huduma za afya katika Vituo vya Afya na Zahanati ambazo ni pamoja na ukosefu wa dawa pamoja na Madaktari jambo linalowasukumba kusaka huduma hizo katika Hospitali za Rufaa ikiwemo Sekour Toure hata kama hawajawapewa rufaa ya kupata matibabu katika Hospitali hizo.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA.

BONYEZA HAPA Kutazama Ziara ya Sekour Toure iilivyokuwa.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.

No comments:

Powered by Blogger.