MWANDISHI WA HABARI SALMA SAID APATIKANA BAADA YA KUTEKWA NA WATU WASIOJULIKANA.
Mwandishi wa habari Salma Said.
Na George Binagi-GB Pazzo kwa Msaada wa Mtandao.
Mwandishi wa Habari wa Idhaa wa
Kiswahili ya Ujerumani ya DW (Deutsche Welle) anaewakilisha Visiwani Zanzibar,
Salma Said, amepatikana baada ya kutekwa na watu wasiojulikana ijumaa
iliyopita.
Jana jioni Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es salaam Simon Siro alithibitisha kupatikana kwa mwandishi
huyo, alietekwa akiwa katika uwanja wa Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es
salaam.
Pia mmewe Salma Said, Ali Salim Khamis amethibitisha kupatakana kwa mkewe na taarifa za awali zinaeleza kuwa Salma hajapatikana na majeraha wala madhara yoyote kutokana na utekaji huo.
Haijulikani Salma alitweka kwa minajiri ipi na wahusika ni akina nani, japo kutekwa kwake kumehusishwa na kazi yake ya
uandishi wa habari ambayo pia huifanya katika magazeti kadhaa hapa nchini na kwamba huenda utekaji huo ulidhamiria kumkwamisha asiripoti habari za Uchaguzi Mkuu wa Marudio Visiwani Zanzibar uliofanyika jana Machi 20.
No comments: