LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC IRAMBA MKOANI SINGIDA AMWOMBA RAIS MAGUFULI KUTOMTEUA KATIKA NYADHFA HIYO TENA.

Na:Shaban Njia
MBUNGE Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga (CCM) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Lucy Mayenga amemwomba Rais wa awamu ya Tano Dkt.John Magufuli kutomteuwa tena katika wadhifa huo kutokan na sababu mbalimbali ikiwemo kukwama kwa biasahara zake.

Mayenga aliyasema hayo katika sherehe za  kutimiza miaka 39 ya Jumuia ya Wazazi (UWT)  Mkoa wa Shinyanga zilizofanyika katika kata ya Nyamilangano katika Halmashauri ya Ushetu Wilayani hapa.

Alisema kuwa kutokana na kubanwa kwa shughuli za kibiashara zake anazozifaya  pamoja na shughuli za kibunge katika Mkoa wa Shinyanga ndizo zimepelekea kumwomba kiongozi huyo wa juu wa Nchi kuachaa kumteuwa kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na vyeo vingine.

“Niliamua kwenda mpaka kwa Rais John Magufuli na kumwonyesha nia yangu ya kutotaka tena kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya katika sehemu yeyote hapa nchini nayeye kama Rais aliniambia kuwa nisubiri mpaka hapo atakapoteuwa tena Wakuu wapya wa Wilaya katika Serikali yake ya awamu ya Tano”,Alisema Lucy Mayenga.

Aidha Mbunge huyo aliendelea kusema kuwa sio kama yeye ameogopa kutokuwepo katika uteuzi mpya bali ameamua kwa Ridhaa yake kuacha Nyazifa hiyo ya Serikali na kuongeza kuwa nguvu kubwa kwa sasa itakuwa katika kuwatumikia Wananchi kama Mbunge pamoja na shughuli zake za kibiashara .

Baadhi ya Wanachama       wa Umoja wa Jumuia ya Wazazi waliokuwepo katika sherehe hizo wakizungumzia kuhusu kauli ya Mbunge huyo walisema kuwa ni bora amejua mapema kuwa hawezi kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kuwataka wengine kama  wanamapungufua wameayaona katika utendaji kazi kuachia ngazi mapema.

“Mimi nimefurahia kitendo cha Lucy Mayenga kuomba mapema kutoteuliwa na Rais Magufuli na Kama kuna viongozi kama hoa wapo ni bora wakawapisha wengine wenye uewezo wa kuongoza Watanzania katika uongozi wa awamu hii ya tano”, Alisema Selina Mkula Mwanachama wa Jumuia ya Wazazi.

Hata hivyo katika Sherehe hizo Jumuia hiyo ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga ilifanikisha kuwapokea Wanachama wapya 56 hali ambayo itachangia katika kuikuza Jumuia hiyo ambayo kwa sasa inakabiliwa na Changamoto nyingi za kuikuza.

Pia katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa alitoa Msaada wa Mifuko 50 katika shule tatu moja ikiwemo ya sekondari na Mbili zikiwa za msingi ili kuinua sekta ya Elimu katika jimbo hilo jipya Wilayani ushetu.

Mifuko  hiyo aliitoa katika shule ya Sekondari ya Nyamilango ambayo ilipata mifuko 10 huku katika shule ya Msingi Mitenga  na Nyamiliangani ikipta Jumla ya mifuko 20 kila moja hali iliyofanya jumla ya mifuko ya Saruji iliyotolewa na Mbunge huyo kufikia 50.

Pia Mbunge huyo alihaidi kutoa Vyerehani 20 kwa makatibu kata wa Umoja wa Jumuia ya Wazazi katika hizo ili kuhakikisha kuwa waanzanzisha shughuli za vitega uchumi katika kata zao hali ambayo itachangia katika kuleta maendeleo katika Jumua hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.