BAADHI WANASHEREHEKEA USHINDI WA CCM VISIWANI ZANZIBAR HUKU UKOSOAJI NAO UKIONGEZEKA.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Jecha Salim Jecha amemtangaza rasmi Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dr.Ali Mohammed Shein kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Zanzibar.
Dr.Shein ametangazwa mshindi hii leo baada ya kupata kura 299.982 sawa na asilimia 91.4 katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana Machi 20,2016.
Vyama kadha vya upinzani ikiwemo chama kikuu cha upinzani Visiwani Zanzibar CUF, vilisusia uchaguzi huo wa marudio kwa madai kwamba vinatambua matokeo ya uchaguzi uliofanyika Octoba 25 mwaka jana ambao matokeo yake yalifutwa kutokana na kuelezwa kukumbwa na mapungufu mbalimbali (kutokuwa huru na haki).
Wakati CCM ikisherehekea ushindi huo, makundi mbalimbali pamoja na wanaharakati wanaendelea kuukosoa uchaguzi huo wa marudio, huku umoja na mshikamano ukiendelea kuhimizwa kwa wakazi wa visiwani Zanzibar.
Soma Zaidi HAPA
No comments: