LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIJANA 30 MAARUFU KAMA TELEZA WATIWA MBARONI MKOANI KIGOMA KWA TUHUMA ZA KUWAINGILIA KIMWILI WAJANE.


Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu 30 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kuwabaka  akinamama wajane na waseja katika mitaa ya Vamia na Katubuka mkoani humo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma SACP, Fredinand Mtui, amesema uhalifu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji  la baadhi ya vijana maarufu kwa jina la teleza kuwaingilia kimwili akinamama na mabinti bila lidhaa yao umedhibitiwa baada ya msako mkali.

Amesema askari polisi walifanya msako katika maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakilalamikia vitendo hivyo ambayo ni Mitaa ya Vamia na Katubuka na kufanikiwa kuwakamata vijana hao ambapo upelelezi bado unaendelea ili kuwabaini wahusika wengine ili waweze kutiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani.

Kamanda Mtui ametoa wito kwa Wananchi wanaojihusisha na uhalifu kuachana na vitendo hivyo na kwa kwamba waendelee kutoa ushirikiano pindi wanapogundua kuna vitendo vya uhalifu vinavyo jitokeza katika mitaa yao.

No comments:

Powered by Blogger.