LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA: TAFUTA NAFASI YAKO.

Ni jambo jema kila mtu kuwa na biashara, lakini ukweli ni kwamba siyo kila mtu anaweza kuanzisha na kusimamia biashara.

Kuna ambao wanaweza kuanzisha lakini hawawezi kusimamia na kuendeleza, pia wapo wasioweza kuanzisha ila wanaweza kusimamia na kuendeleza.

Hii ipo mpaka kwenye ajira, sio kila mtu ni muajiri wengine ni bora sana kwenye kuajiriwa, katika mazingira ya namna hii tafuta mtu ambaye anaweza kufanya kile ambacho wewe huwezi siyo kila  kitu utaweza kukifanya peke yako.

Na utu uzima wangu huu nimekuja kugundua hakuna kitu kinachoumiza na kumchanganya mtu kwenye maisha kama kufanya kazi kwa bidii halafu unakosa cha kuonesha (matokeo duni).

Siyo mvivu, unafanya kazi kwa bidii, unajituma, ni mkweli, ni mkarimu, unafanya mambo yako katika hali ya juu kabisa lakini hakuna matokeo mazuri kama hili linakutokea linaweza kuwa linasababishwa na mambo yafuatayo...

i)Hauna nia ya kutosha kwenye suala unalolifanya, yaani unafanya tuu sababu hauna kitu kingine cha kufanya.

ii)Unafanya lakini haufurahii kile unachokifanya hivyo unakosa ubunifu.

iii)Haufanyi kusudi lako, unafanya jambo ambalo hukuumbiwa kufanya.

iv)Hujakutana na mtu/watu sahihi wa kukuunganisha na mtu ambaye atanyoosha njia yako.

Binafsi nina ubora baadhi ya sehemu na ni dhaifu kwenye sehemu nyingine na ninalijua hili, uzuri ni kwamba huwa sihangaiki na udhaifu wangu napalilia ubora niliokuwa nao huku ninasaidiana na watu wengine kuziba udhaifu niliokuwa nao.

Jua kwamba kama kuna kitu kinakukereketa sana katika jamii yako  hapo ndipo Mungu alipokuitia upatengeneze pawe vyema.

Katika maisha mtu huinuliwa kwa matatizo anayoyatatua siyo kwa malalamiko anayotoa, hivyo acha kulalamika sababu hutafika mahali popote pale bali chukua jukumu la kutatua matatizo.
The time to be a winner is NOW!
Hamphey Makundi, Mdau.

No comments:

Powered by Blogger.