LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mstaafu Dar aanza ufugaji wa samaki, vijana watakiwa kuiga mfano wake

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, BMG
Wananchi hususani vijana wametakiwa kujikita kwenye shughuli za ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba na mabwawa, ili kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuongeza pato la taifa kupitia sekta hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Rashid Tamatamah aliyasema hayo alipotembelea kampuni ya Meck Fish Farm inayomilikiwa na aliyewai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki iliyopo Kamanga Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

"Njia bora ya kuongeza pato la taifa ni ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kwa walio na maji kama ziwa na bahari  kwani ina faida mara kumi zaidi”. Alisema Tamatamah.

Naye mmiliki wa Meck Fish Farm, Saidi Meck Sadiki alisema amejifunza ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba katika nchi za Kenya, Uganda na China na kubaini kwamba una manufaa zaidi ambapo hadi sasa ana vizimba 32 huku malengo yakiwa ni kufikia vizimba 52 ambapo kila kizimba kina uwezo wa kubeba samaki elfu kumi na saba (17,000).

No comments:

Powered by Blogger.